Header Ads Widget

RC BABU APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI WA ZAO LA TANGAWIZI KIHOLELA.

 


 WILLIUM PAUL, Same.


SERIKALI mkoani Kilimanjaro imesema haitamvumilia mkulima yeyote atakayeuza zao za tangawizi  nje ya kiwanda Mamba Miamba Ginger Growers.


Pia  wawekezaji wa kiwanda hicho Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF),  wametakiwa kuona namna yakuongeza bei ya zao hilo kwa kilo.



Hayo yamesemwa na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu jana katika hafla ya uzinduzi wa ukarabati wa Kiwanda cha kuchakata Tangawizi cha Mamba Miamba Ginger Growers kilichoko wilayani Same mkoani hapa ambapo aliyemwakilisha     Rais Dkt. Samia Suluhu Hasan.


Alisema uwekezaji uliofanyika katika kiwanda hicho  uliwekwa kwa lengo la kukuza kipato cha mkulima wa tangawizi  hivyo ni wajibu wa kila  mkulima kuhakikisha anapeleka tangawizi hapo.



“Kiwanda hiki kinamilikiwa kwa ubia kati ya PSSSF na Ushirika wa wakulima wa tangawizi wa Mamba Miamba Ginger Growers ambapo PSSSF inamiliki asilimia 67% ya hisa na wanaushirika wanamiliki asilimia 33%,  hatutapenda kuona  wakulima wanasumbuka na bei" alisema Babu.


Na kuongeza "Hatupo tayari kuona mali ghafi zinapelekwa nje ya nchi kinyume na taratibu kanuni na sheria tulizojiwekea,  ni lazima mkumbuke kiwanda hiki  kitatuongezea ajira kwa vijana wetu na kukuza uchumi wa taifa letu,”alisema



Naye Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF,  Hosea Kashimba alisema uwekezaji uliofanywa na Mfuko huo umefanyika kwa kufuata miongozo ya Benki Kuu pamoja na Sera ya Uwekezaji ya Mfuko.


“Lengo kuu likiwa ni kuwa na uendelevu wa kifedha ili kulinda thamani ya fedha za wanachama na lengo lingine ni kupata faida ya uwekezaji ili kukuza hazina na kuongea uwezo wa kulipa Mafao pale yanapohitajika na pia kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika nchi.”



 Kashimba alisema kiwanda hicho kilijengwa mwaka 2012 lengo likiwa ni kusindika tangawizi kiasi cha tani 9.8 kwa siku jambo ambalo halikuwezekana na kiwanda kilizalisha chini ya tani moja kwa siku kinyume na matarajio sababu kubwa ikiwa ni uwezo mdogo wa mitambo.


“Kutokana na sababu hiyo wanaushirika kupitia Mbunge wa jimbo la Same Mashariki Anne Kilango uliomba ubia na PSSSF na baada ya kufanyika uchambuzi Mfuko ulikubali kuingia ubia na kuanza ukarabati wa majengo na ufungaji wa mashine mpya za kisasa uliogharibu karibu shilingi Bil mbili" alisema Kashimba.


Na kuongeza "Kiwanda hiki kwa sasa kinauwezo wa kuzalisha tani 10 kwa siku na kina maabara za kisasa zenye kukidhi viwango vya kimataifa kwa kupima ubora wa tangawizi inayozalishwa kiwandani.” Alifafanua Kashimba.


Aidha akitoa salamu za wilaya hiyo mkuu wa wilaya ya  same,  Edward Mpogolo alisema kukamilika kwa kiwanda hicho kitaweza kusaidia wakulima  kupata soko la uhakika litakaloweza kuwanyanyua kiuchumi.



“Ndugu zetu wa PSSSF wametusaidia kuboresha zao la Tangawizi kwa kutuletea kiwanda na imani yetu kubwa sana wana Same na hususan sisi wakulima wa zao la Tangawizi watatusaidia kutengeneza soko na kuboresha bei ya Tangawizi katika maeneo yetu na Tanzania kwa ujumla.” alisema Mpogolo.

Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki, Anne Kilango Malecela kuwa, maono yake ilikuwa ni kujenga kiwanda cha kuchakata Tangawizi katika kata ya Miamba ambapo PSSSF wametimiza ndoto yake hiyo.


Anne Kilango alisema kuwa, wananchi wa Jimbo hilo ni wakulima wazuri wa zao la Tangawizi hivo kupatikana kwa kiwanda hicho kitawanufaisha wakulima kupata soko la uhakika na kujiinua kiuchumi.

Aidha Mbunge huyo alitumia nafasi hiyo kuiomba Serikali kuona umuhimu wa kuijenga barabara ya Ndungu-Miamba kwa kiwango cha lami ili kuwezesha magari kufika kiwandani na kusafirisha bidhaa kwa wepesi mpaka sokoni.

Mbunge huyo alidai kuwa, wananchi wa Jimbo la Same mashariki wamenifaika kwa fedha za tozo na kuipongeza Serikali kwa jinsi ambapo imetekeleza miradi mbalimbali.
 
Nao baadhi ya wakulima akiwemo mwanzilishi wa zao hilo wilayani hapo  Kilango Mfanga alisema kiwanda hicho kimeleta faraja kubwa kwa wakulima yeye akiwemo.

 

“Niliingiza mbegu ya Tangawizi kwenye eneo hili mwaka 1988 na niliweza kuuza maeneo mbalimbali ya nchi ikiwemo Arusha,

Mwisho..

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI