Header Ads Widget

DC MTWARA APONGEZA TPDC

 




Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Dunstan Kyobya amelipongeza Shirika la Maendeleo ya Petrol Tanzania (TPDC)  kwakutoa msaada wa pikipiki kwa ofisi ya tarafa ziwani ili kurahisihsa usafiri kwa watumishi wa ofisi hiyo.



Akipokea pikipiki hiyo alisema kuwa tarafa hiyo ni kubwa na ina miundombinu yote ya gesi hivyo usafiri huo utasadia hasa utolewaji wa elimu ndani ya kata hiyo inayohusu gesi.


“Nashukuru TPDC kuleta kitendea kazi ambacho kitasogeza huduma kwa wananchi hii tarafa ina kata nane yaani ni Asilimia 99 ya gesi ndni ya mkoa huu Mtwara inatoka tarafa ya ziwani kupatikana kwa usafiri huo kutamwezesha afisa tarafa kuzunguka na kuangalia vitu mbalimbali ikiwemo miundombinu ya gesi”


Nae Katibu Tawala wa Wilaya ya Mtwara Thomas Salala alisema kuwa usafiri huo utaongeza uwajibikaji kwa afisa tarafa wa ziwani.


“Ili aweze kutekeleza majukumu kwa haraka amepatiwa usafi tutawajibika iweze kuendelea kuwepo na kuiwezesha mambo ya msingi ili mtendaqji aweze kuifikia jamii kubwa zaidi ndnai ya tarafa ya ziwani”



Nae Afisa Tarafa Ziwani Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Winifrida Linyembe alisema kuwa anashukuru  kwa TPDC kwakumuwezesha kupata usafiri huo ambao utamuwezesha kufika kata mbalimbalizilipo kwenye tarafa hiyo.


“Nitafanyakazi kwa uadilifu kwakuwa nimewezeshwa usafiri tarafa yangu ni kubwa kata 8 vijiji 48 hivyo usarifi ilikuwa ni changamoto kwangu kuweza kuzifikia kata hizo na vijiji”


Akikabidhi Pikipiki hiyo Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TPDC James Mataragio, Mhandisi Kassimu Mkombwa alisema kuwa wameona umhimu wa afisa tarafa huyo kupata usafiri kutokana na ukubwa wa tarafa hiyo.



“Tumekuwa tukitoa misaada mbalimbali kwa jamii kama sehemu ya kurudisha faida kwa jamii ndio maana tulipopokea taarifa hii tuliona kuna umuhimu mkubwa wakulitekeleza ili kumrahisishia Afisa tarafa kwenda katika maeneo mbalimbali”


“Unajua tunayomaeneo mbalimbali yamepitiwa na bomba la gesi hivyo upatikanaji wa pikipiki hiyo utasaidia kusafiri na kuyafikia maeneo hayo kwa urahisi” alisema Linyembe

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI