Header Ads Widget

ZAINABU VULLU ASHINDA UENYEKITI UWT MKOA WA PWANI.

 




ALIYEWAHI kuwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani Zainabu Vullu amefanikiwa kushinda kwenye uchaguzi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa huo baada ya kupata ushindi wa kishindo kwa kupata kura 320 dhidi ya kura 38 za mshindi wa pili.


Uchaguzi huo ambao ulisimiwa na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Zainabu Abdala, ulifanyika Mjini Kibaha ulimrudisha Vullu kwenye nafasi hiyo ambayo aliwahi kuishika miaka mitano iliyopita na kushikiliwa na Farida Mgomi aliyemwachia Vullu.


Vullu alimshinda mshindani wake aliyemfuata Joan Tandau ambaye alipata kura 38 akifuatiwa na Rehema Ngatunda aliyepata kura 1 na Safihuna Singo aliyepata kura 1 kati ya kura 358 zilizopigwa ambapo hakuna kura hata Moja iliyoharibika.


Kwa upande wa mwakilishi wa baraza kuu la mkoa kwenda Taifa Mariamu Ibrahimu ameshinda kwa kupata kura 188 nakumshinda Nancy Mutalemwa aliyepata kura 165


Mwenyekiti huyo amesema baada ya kushinda nafasi hiyo atafuatilia suala la asilimia 10 ya mikopo inayotolewa na Halmashauri za Wilaya.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS