Header Ads Widget

WANALINDI WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA MASOMO VETA

 



 NA HADIJA OMARY LINDI....



WANANCHI Mkoani Lindi wametakiwa kuchangamkia fursa ya uwepo wa chuo cha ufundi stadi VETA - Lindi kwenda kupatiwa mafunzo katika fani mbali mbali zinazotolewa chuoni hapo.



Wito huo umetolewa na Mbunge jimbo la Lindi mjini mheshimiwa Hamida Abdallah katika sherehe za mahafali ya 9 ya wahitimu wa mafunzo ya ufundi stadi VETA yaliyofanyika katika viwanja vya chuo hiko mapema leo November 17,  2022.



Hamida alisema kuwa licha ya uwepo wa chuo hiko cha VETA katika Mkoa huo lakini bado inaonyesha wananchi wa Lindi bado hawajahamasika vya kutosha kujiunga na mafunzo yanayotolewa chuoni hapo.



Alisema licha ya chuo hiko kuwa na uwezo wa kudahili wanafunzi 506 lakini hadi hivi sasa kimedahili wanafunzi 392 idadi ambayo ipo chini ukilinganisha na uwezo wa chuo hiko.



Alisema kitendo cha Wazazi na walezi wa Mkoa huo kutoona umuhimu wa kuwekeza kwa watoto wao kwa kuwapeleka kupata ujuzi na maarifa kutawafanya vijana hao kukosa utayari wa kushiriki katika ujenzi kupitia uwekezaji.



Mhe. Hamida aliongeza kuwa ni wajibu wa Wazazi na Walezi kuwahamasisha na kuwasimamia watoto wao ili watambue umuhimu wa mafunzo ya ufundi stadi katika kuwajengea uwezo wa kujiajiri na kuajiriwa katika kutekeleza dhana ya serikali ya awamu ya sita .




" niwaombe wananchi wa Mkoa wa Lindi na Wilaya zake , fursa hii imetufikia tusipoitumia watatoka watu kutoka mbali kuja kunufaika na chuo hiki nasi kubaki watazamaji na wasikilizaji pale fursa za uwekezaji zitakapojitokeza mkoani kwetu" alisema mhe. Hamida.




Aidha mhe. Hamida pia  alisema kuwa kwa kutambua fursa za ajira zilizopo kutokana na uwekezaji mkubwa unaofanyika katika sekta ya Gesi na Mafuta na viwanda vingine katika Mikoa ya Lindi na Mtwara, aliusihi   uongozi wa chuo hiko cha VETA Lindi kuhakikisha unaongeza ubora wa mafunzo wanayoyatoa ili Ajira hizo zinapotokea zisije chukuliwa na wageni.



Awali akitoa Taarifa ya chuo Mkuu wa chuo cha Ufundi stadi VETA Lindi mhandisi Harry Mmary alisema kuwa kwa mwaka 2022 chuo hiko kimeweza kuongeza udahili wa wanafunzi 185 kati ya wanachuo 506 waliohitajika katika fani kumi na moja  kwa wanachuo wa mwaka wa kwanza.




Alisema  katika kipindi cha mafunzo mwaka 2022 chuo hiko kilikuwa na uwezo wa kudahili wanafunzi 506 lakini waliweza kudahili wanafunzi 392 wakiwa ni pungufu ya wanafunzi 114 sawa na asilimia 22.5% ambapo juhudi kubwa zinahitajika za kutoa elimu kwa jamii ya watu wa Lindi juu ya kuzitumia fursa hizo za mafunzo kupitia chuo hiko.



Hata hivyo Mmari alisema kuwa chuo hiko kimeendelea kushirikiana na wizara , mashirika mbali mbali  pamoja na Taasisi zisizo za kiserikali kuendesha progamu za kimafunzo katika kuwawezesha vijana wa mkoa huo wa Lindi kujiimarisha kiuchumi.



" kupitia ofisi ya Waziri Mkuu sera , vijana  Ajira na wenye ulemavu kwa kushirikiana na shirika la maendeleo la ujerumani (GIZ) kutekeleza mradi wa kukuza ajira na ujuzi kwa maendeleo (E4D) tunajiandaa kutoa mafunzo ya ujenzi katika fani za  uchomeleaji vyuma viwandani, ufundi bomba wa viwandani na majumbani, kwa vinana 700 mafunzo ambayo yataendeshwa kwa njia mbili  yaani mfumo wa kawaida  wa kusoma chuoni na mfumo wa kutumia mtandao kupitia VSOMO" alifafanua mmari.




Kupitia lisala ya wanafunzi wahitimu wa mafunzo ya ufundi stadi wa  ngazi ya pili na tatu  iliyosomwa na  Athumani Mtao Alisema kuwa  matarajio yao ni kupata ajira mara baada ya kuhitimu mafunzo hayo ya ufundi husisani kwenye makamuni ya mafuta na gesi pindi vikianza uzalishaji hiyo ni kutokana na ukanda wa kusini kupata fursa ya uvumbuzi wa mafuta na gesi , na kupelekea makampuni mengi ya ndani na nje ya nchi kuja kuwekeza upande wa kusini mwa Tanzania



Pia alisema kuwa sambamba na matarajio ya hayo wahitimu hao wapo tayari kujiajiri wenyewe kupitia taaluma zao za kiufundi walizojifunza chuoni hapo hasa pale nafasi za ajira katika sekta mbali mbali zitakapokosekana.





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS