Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Watumishi wa mamlaka ya mapato Tanzania TRA wametakiwa kuacha vitendo vya udanganyifu wakati wa ukadiliaji wa kodi kwa wafanyabiashara kwani vinasababisha serikali kukosa mapato mengi.
Katibu tawala Wilaya ya Njombe Emmanuel George kwa niaba ya mkuu wa mkoa katika maadhimisho ya wiki ya shukrani kwa mlipa kodi amesema TRA wanapaswa kuonyesha uzalendo kwa kuacha vitendo vya kuingia makubaliano na wafanyabiashara kuiibia Serikali mapato.
Aidha Bwana George amewataka TRA kuwaeleza wananchi kodi zao zinafanya nini na Kuna faida gani na hasara gani za kulipa na kutolipa kodi.
Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa amesema kinachotakiwa katika ukusanyaji kodi ni uzalendo kwa watumishi wenyewe,Wananchi na hata wafanyabiashara hivyo kila mmoja anapaswa kuwajibika katika majukumu yake.
0 Comments