Header Ads Widget

MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BIMA (TIRA) KUTOA ELIMU KWA WANANCHI MKOANI MWANZA

.

Kaimu Meneja wa Kanda ya Ziwa (TIRA) Richard Toyota
Meneja maendeleo ya Soko la Bima kutoka (TIRA) Stella Rutaguza

xxxxxxxxxxxxxxxx

NA CHAUSIKU SAIDMATUKIO DAIMAAPP MWANZA

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) imewataka wananchi Mkoani Mwanza kujitokeza katika maonesho ya wiki ya huduma za kifedha ili kupata elimu ya namna bima inavyofanya kazi katika nyanja mbalimbali.


Hayo yamebainishwa na Kaimu Meneja wa Kanda ya Ziwa Richard Toyota na kueleza kuwa  Kuna umuhimu wa wananchi kuendelea kupata elimu ya bima kutokana na majanga mbalimbali yanayotokea.


Toyota amesema kuwa bado Kuna changamoto ya uelewa wa maswala ya bima kwa wananchi hali inayopelekea kupata majanga mbalimbali ikiwemo kuunguliwa na nyumba, na kushindwa namna ya kutatua.


"Sisi Kama Mamlaka ya bima uwepo wetu hapa ni kuhakikisha wananchi wanapata bima hata wanapokuwa kwenye shughuli zao za kiuchumi wanakuwa salama Kwa kuwa na Kinga ya vitu vyao" Alisema Toyota.

 

Kwa upande wake Meneja wa Maendeleo ya Soko la Bima kutoka (TIRA) Stella Rutaguza amesema kuwa wanatoa elimu Kwa wananchi kuhusu haki na wajibu wa mteja wa bima namna ya kufuata utaratibu pindi anapokuwa na madai au anatakiwa kupata fidia.


"Sisi Kama Mamlaka ya usimamizi wa bima tuko hapa kuwaeleza wateja wetu utaratibu wote namna ya kupata huduma Bora" Alisema Rutaguza.


Rutaguza amesema kuwa Baadhi ya wananchi wameona  umuhimu wa bima wameweza kujiunga zao Kwa faida ya kiuchumi na kijamii.


"Ukiwa na bima hautakuwa na wasiwasi wa janga lolote litakalotokea na kuwaza utaanzia wapi baada ya janga lililokupata ukiwa na bima tutakufidia na wewe utaendelea na shughuli zako za kiuchumi" Alisema





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI