Header Ads Widget

VYAMA TISA VYA UPINZANI VIMELAANI KAULI YA CHAMA CHA ACT WAZALENDO

 


VIONGOZI wa Vyama Tisa vya Siasa vya Upinzani Visiwani Zanzibar, vimesema Vinalaani Vikali kauli ya iliyotolewa na  Chama Cha Act Wazalendo  yakumtaka Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dkt  Hussein Ali Mwinyi kutengua uteuzi wa mkurugenzi wa uchaguzi katika tume ya uchaguzi ya Zanzibar alioufanya hivi karibuni.


Hayo wameyaeleza leo Wakati wakizungumza na Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Kikwajuni Mjini Unguja ambapo wamesema kitendo hicho ni kinyume na Kanuni na Taratibu za Nchi.


Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia Makini  Ameir Hassan Ameir amesena kuwa Chama cha ACT Wazalendo hakina Mamlaka ya kupinga Uteuzi wa Rais kwa Mujibu wa Sheria na Kanuni za Vyama vya Siasa pamoja na Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984.


Amesema ACT walipaswa kupeleka mapendekezo yao katika Kamati iliyoundwa na Rais juu ya Kushughulikia masuala ya Kisiasa Zanzibar na hawakupaswa Kujitokeza wazi wazi kupinga Uteuzi wa Rais.


“Kwa Mujibu wa Kanuni na Sheria za Nchi Rais ndiye kiongozi Mkuu wa Nchi hivyo ukiwa na jambo lolote katika Kumshauri Rais unapaswa kufuata kanuni na Taratibu kinyume chake ni kumvunjia heshima na kukiuka taratibu za Nchi,” alieleza.


“Tabia zetu ni kuheshimu viongozi na watu wazima na kama unamshauri ni kupitia taratibu za kiheshima sio kutoa amri mitandaoni. Inasikitisha sana kuona chama ambacho kina kiongozi mkubwa tu katika Serikali kinakurupuka kwenye mitandao kutoa maagizo kwa Kiongozi mkuu wa Nchi badala ya kumtumia yeye kupeleka ushauri au maoni,” alifafanua.


Aliongeza kwa Kumpongeza Rais wa Zanzabar na Mwenyeiti wa Baraza la Mapinduzi kwa Kazi mbalimbali anayoifanya katika kuleta maendeleo ya Wazanzibar.


“Mimi nachukua fursa hii kumpongeza Rais kwa kazi kubwa ambayo anaifanya ili kuhakikisha Wazanzibar wanapata Maendeleo, Wito wangu kwake aendelee kutekeleza dhama yake njema kwa Wazanzibar,” alieleza.


Nae katibu Mkuu wa Chama cha UPDP Hamad Mohammed Ibrahim alieleza kuwa, kitendo kilochofanywa na chama Cha ACT Wazalendo ni kitendo cha makusudi ambacho dhamira yake ni kuleta mtafaruku katika nchi na kuchafua jina la Mkurugenzi wa Uchaguzi Thabit Idarous Faina.


Alieleza chama hicho kinapaswa kujitokeza hadharani kuomba radhi kwa kumdhalilisha na kumgombanisha na Jamii Rais wa Zanzibar Dkt Hussein Ali Mwinyi.


“Sisi vyama vya Siasa tunapaswa kuwa Mstari wa mbele katika kuhakikisha tunaunganisha jamii na si kuleta mtafuruku kwa jamii, wanapaswa kujitokeza kuomba radhi kinyume na hapo chama hicho kitaonyesha kwa jamii namna kilivyokosa muelekeo wa kuwa chama cha kisiasa,” alisema.


Katika Maelezo yake alisema kuwa Chama cha ACT Wazalendo hawakupaswa kutoa taarifa ambayo inawaelezea Wanzanzibar wote kuwa hawakutaka Uteuzi wa Thabit Idarous Faina.


“Mnasema Wazanzibar hawamtaki Faina, ni wangapi? Mumewauliza saa ngapi hata ingekuwa mnazungumzia hao wanachama wenu tu je? mmewauliza saa ngapi, au imekaa timu ya watu wachache wanaandaa uchochezi katika chama chenu na kulivaa koti la Wanzibari, kitendo hicho ni ishara uchochezi,” alieleza.


















Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI