Teddy Kilanga, Arusha.
Tanzania kuwa mwenyeji wa maadhimisho ya miaka 50 ya mkataba wa Shirika la umoja wa mataifa unaoshughulikia masuala ya elimu,Sayansi na utamaduni(UNESCO)wa mwaka 1972 kutokana na kukidhi vigezo vyote vilivyoweka na umoja wa mataifa katika makubaliano ya utekelezaji wake.
Maadhimisho hayo yanatarajiwa kufanyika Desemba 12 hadi 14,2022 jijini Arusha ambayo yameandaliwa na UNESCO kwa kushirikiana Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro(NCAA) yenye mlengo wa kujadili utekelezaji wa mkataba huo katika masuala ya urithi wa asili na utamaduni kwa kuwaleta pamoja wataalamu mbalimbali kutoka nchi 52 duniani.
Akizungumza na vyombo vya habari,jijini Arusha mkuu wa kitengo cha sayansi asilia kutoka UNESCO Kelvin Robert amesema vigezo hivyo ni pamoja na kuaminika katika mtiririko wa dunia katika usawa wa mazingira na utamaduni.
"Pia kigezo kingine cha Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano huu ni kutokana na kuridhia mkataba huu nakuanza kuutekeleza tangu mwaka 1977 pasipokuwa na migogoro ya aina yoyote,"amesema Robert.
Robert amesema Tanzania kuwa mwenyeji wa maadhimisho hayo ni fursa katika kuleta nchi za kiafrika kufika nchini kujifunza namna njema walivyotekeleza mkataba huo pamoja na kubadilishana changamoto zinazoikabili ikiwemo wataalamu wa kutosha.
"Ni fursa nzuri kwa Tanzania kuweza kuielimisha dunia na wadau mbalimbali kuhusu mbinu na mikakati iliyoweza kutumika hifadhi ya Ngorongoro inavyosimamiwa kikamilifu kwa kutekeleza mkataba wa mwaka 1972 katika nyanja ya mawasiliano,uwajibikaji,uhifadhi,kujenga uwezo na ushiriki wa jamii,"amesema.
Aidha amesema katika nchi ya Tanzania jumla ya hifadhi saba zipo katika urithi wa kidunia ikiwemo mlima kilimanjaro,Pori la akiba Silui,Serengeti,Mji wa mawe(Stone town) ,Kilwa kisiwani,Kondoa,Songo mnara pamoja na kazi za sanaa Kondoa(Kondoa Art works).
Kwa upande wake Kamishna Msaidizi mwandamizi Mhadhiri Joshua Mwankonda amesema nchi ya Tanzania imekuwa ikinufaika na mkataba wa urithi wa asili na kiutamaduni katika kujitangaza hali inayosaidia kuongeza watalii katika hifadhi ya Ngorongoro hivyo matarajio yao ni kuongeza ubora wa kiwango cha uhifadhi.
0 Comments