Naibu Waziri Maendeleo ya Jamii, Jinsia,wanawake na makundi maalumu Mhe. Mwanaidi Ali Khamis amepongeza chuo Cha maendeleo ya Jamii Ruaha mkoani Iringa Kwa mapambano dhidi ya udumavu na utapiamlo .
Akitoa pongezi hizo Leo wakati wa Mahafali ya 14 ya chuo hicho Naibu Waziri huo amesema jitihada kubwa zimefanywa na chuo hicho Katika utoaji elimu ya lishe Kwa jamii inayozunguka .
Hata hivyo amepongeza menejimenti ya chuo Kwa kuendelea kuimalisha Mapato ya ndani Kwa kubuni vyanzo vya Mapato kama ugugaji samaji ,uchakataji ngozi na shughuli nyingine za Kiuchumi .
Alisema alipofika chuoni hapo alitembelea mabwawa ya samaki na kuona jitihada hizo kubwa ambapo kupitia ugugaji huo wananchi watapata Afya Bora .
Aidha alipongeza chuo Kwa kupata kibali Cha utafiti wa lishe Iringa na kuagiza vyuo vingine kuandika maandiko ya kazi mbali mbali za chuo Kwa lengo la Kutangaza chuo .
Akielezea changamoto za chuo hicho kama Nyumba za walimu na Mabweni alisema changamoto hizo amezichukua na atakwenda kuzifanyia kazi .
Pia alisema suala la miundo mbinu ya barabara atauagiza uongozi wa mkoa ili kuboresha mazingira ya chuo hicho .
Huku akiwataka wahitimu wa chuo hicho kutumia vema mafunzo ambayo wamepata Kwa kwenda Vijijini kuwatumikia wananchi.
Alisema Rais Samia Suluhu Hassan ameunda wizara ya maendeleo ya Jamii ili kusaidia jamii kupata elimu Bora .
"Ndugu wahitimu mtakapopata fursa ya kupata kazi jiepusheni na vitendo vya Rushwa na miawe mabalozi mazuri wa kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia"
"Tumekuwa tukifanya kazi kwa ushirikiano wa karibu na nimekuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono juhudi za Chuo katika utekelezaji wa majukumu yake, ninaahidi kutimiza wajibu wangu nikiwa kama Naibu Waziri, kwa kutoa msaada pale itakapohitajika na nitakapoona inafaa".
Alisema anatambua kuwa ili kuweze kufikia malengo waliyojiwekea katika kutekeleza mpango mkakati wa Chuo, ni lazima kuwe na juhudi za makusudi za kuhakikisha upatikanaji wa fedha za maendeleo.
" Nitajitahidi kwa kadri ya uwezo wangu kwa kushirikiana na Wizara yetu pamoja na Wizara ya Fedha kuhakikisha suala la upatikanaji wa fedha za kutosha za ruzuku na miradi ya maendeleo kwa ajili ya uendeshaji wa Chuo hiki linapewa kipaumbele Ndugu Wahitimu, Napenda nitumie fursa hii kuwapongeza sana wote ambao mtatunukiwa hivi punde Stashahada na Astashahada za Maendeleo ya Jamii. Niwapongezeni sana kwa juhudi kubwa mliyoonyesha katika kipindi chote mlichokuwa hapa Chuoni, kilichowapelekea kufikia mahafali ya siku ya leo"
Aidha alisema anatambua umuhimu wa elimu ya Maendeleo ya Jamii katika maendeleo ya ulimwengu wa sasa; napenda niwasisitize umuhimu wa kujiendeleza katika fani hii ili muweze kuwa chachu ya mabadiliko chanya ya kimtazamo wa jamii.
Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan anachukizwa Sana na vitendo vya ukatili vinavyojitokeza Katika jamii yetu hivyo ni jukumu lenu kwenda kulifanyia kazi janga la ukatili Kwa kutoa elimu Bora na wale wanaopata msongo wa mawazo Kwa kufanyiwa vitendo vya ukatili mkawasaidie kuwapa elimu.
Awali mkuu wa chuo hicho Godfrey Mafungu alipongeza Serikali Kwa kuendelea kutoa fefha za maboresho Katika chuo hicho na kuwa pamoja na jitihada hizo kuwa zipo changamoto za Nyumb a za walimu na ma b mabweni.
0 Comments