Header Ads Widget

SILAHA HARAMU KUTEKETEZWA JIJINI DAR ES SALAAM

 Jeshi la Polisi nchini limesema Novemba 22, 2022 litateketeza silaha haramu zilizosalimishwa kwa hiari katika kampeni maalumu iliyofanyika nchi nzima kuanzia Septemba 01, 2022 hadi Oktoba 31, 2022 iliyokuwa ikiongozwa na kauli mbiu isemayo Silaha haramu sasa basi, salimisha kwa hiari.

 

Taarifa hiyo imetolewa Novemba 20, 2022 na Msemaji wa Jeshi la Polisi Kamishina msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP DAVID MISIME ambapo amebainisha kuwa zoezi hilo litafanyika kuanzia muda wa saa 02:00 asubuhi katika Viwanja vya shabaha vya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) vilivyopo Kunduchi, jijini Dar es Salaam.

 

Aidha amebainisha kuwa Mgeni rasmi katika zoezi hilo anatarajiwa kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Jumanne Sagini (Mb).

 

SACP Misime amesemaa kuwa Jeshi hilo linawaalika wananchi Pamoja na Viongozi wa Serikali za mitaa hususani wanaoishi maeneo ya Kunduchi kuhudhuria ili kujionea mafanikio makubwa yaliyopatikana kutokana na kampeni hiyo ya usalimishaji silaha.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI