Na Lucas Raphael,Tabora
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Tabora Polytechnique College (TPC) Msimamizi wa Uchaguzi huo Martin Shigella alisema Wakasuvi amepata zaidi ya asilimia 90 ya kura zote.
Alibainisha kuwa nafasi hiyo ilikuwa na wagombea 3, Waziri Jumbe, Stella Enock na Hassan Wakasuvi lakini wakati wakijinadi mbele ya wapiga kura, mgombea Waziri alijitoa katika kinyang’anyiro hicho na kumuunga mkono Wakasuvi.
Aliongeza kuwa licha ya mgombea huyo kutangaza kujitoa bado alipigiwa kura 14 na baadhi ya wajumbe huku Stella akipata kura 80 na Wakasuvi kura 1030 kati ya kura zote 1124 zilizopigwa.
Aidha katika uchaguzi huo Mohamed Hamdan Nassoro (Meddy) alichaguliwa kwa kishindo kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC) baada ya kupata asilimia 90.6 ya kura zote na kuwaacha wapinzani wake mbali sana.
Kwa upande wa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ngazi ya Mkoa, waliochaguliwa kwa kila wilaya ni Alcard Ilagila na Leonard Amando (Urambo), Iddy Moshi na Razack Juma ( Uyui) na Lucas Selelii na Getrude Pius (Nzega).
Wengine ni John Kadutu na Denis Lugina Kilatu (Kaliua), Regina Tadeo na Aneth John (Igunga), Jaha Kaducha na Zabibu Nyamwelu (Tabora mjini) na Said Maulid na Alijah Mwiga (Sikonge).
Shigella alipongeza Sekretarieti ya Mkoa na Mkurugenzi wa Uchaguzi huo ambaye ni Katibu wa CCM Mkoa Elias Mpanda kwa kuratibu vizuri na kufanikisha zoezi la uchaguzi huo kwa weledi mkubwa.
Naye Mwenyekiti Wakasuvi aliwapongeza wajumbe wa mkutano huo na wanaCCM wote kwa imani kubwa waliyonayo kwake na kuwataka kuendelea kudumisha umoja na mshikamano ili chama kiendelee kukubalika na jamii nzima.
Kwa upande wake Mohamed Nassoro Hamdan (MNEC) aliwapongeza wanaCCM wa Mkoa huo kwa kumchagua Wakasuvi kuwa Mwenyekiti wa chama hicho na kuahidi kushirikiana naye ili kukiletea mafanikio makubwa chama hicho.
Baada ya uchaguzi huo Halmashauri Kuu ya Mkoa iliketi na kuwachagua Iddy Moshi, Janath Kayanda na Lucas Selelii kuwa Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa ambao wataungana na Mwenyekiti na Katibu wa CCM Mkoa, Mwenyekiti wa Wazazi, UWT na UVCCM na Mkuu wa Mkoa.
0 Comments