Header Ads Widget

ASIYEFAHAMIKA AFARIKI BAADA YA KUJITUPA BWAWANI KIBENA NJOMBE

Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE

Mwanaume ambaye hajatambulika majina yake amefariki baada ya kujirusha kwenye maji katika bwawa dogo lililopo kwenye msitu wa TANWAT halmashauri ya mji wa Njombe huku sababu za kijana huyo kujirusha kwenye maji zikishindwa kufahamika.


Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo ambao ni walinzi wa maeneo ya misitu akiwemo Godfrey Mpolya na Jelio Mtagawa wanasema majira ya saa kumi na moja alfajiri waliona mtu akishuka na tochi katika eneo  la bwawani na kujirusha kwenye maji na walipofika kumzuia ikashindikana.


Mtaalamu wa uogeleaji toka jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Njombe Fedrick Kanoni amesema walipoingia kwenye maji huyo walimkuta akiwa ameshafariki.


Kaimu kamanda wa jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Njombe Inspector Joel Mwakanyasa amesema kijana huyo anakadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 30-35 na hajafahamika shughuli yake wala alikotokea hivyo jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi zaidi.


Inspector Mwakanyasa ametoa onyo kali kwa watu wanaosogea kwenye maji yenye kina kirefu ilihali hawajui kuogelea na kwamba ni marufuku kusogelea maeneo hayo.








Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI