Wakati
Mbunge wa Kigamboni, Dk Faustine Ndugulile akiiomba Serikali kuangalia upya
tozo katika Daraja la Kigamboni, Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuendelea
kutozwa akiwataka wananchi wajenge mazoea hayo.
Katika
msisitizo wake, Rais Samia amesema tozo hiyo inatokana na deni la gharama za
ujenzi wa mradi huo hivyo hakuna mwingine wa kulipa isipokuwa wananchi wenyewe.
Awali,
akitoa salamu katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa maji Kigamboni, ugawaji
vifaa vya uchimbaji visima na makabidhiano ya eneo la bwawa la Kidunda kwa
mkandarasi Sino Hydro, Dk Ndugulile amemuomba Rais Samia kuangalia utaratibu wa
kutoa tozo hiyo.
“Kigamboni
unaingia kwa hela kila siku na lazima urudi kwa hela, kwa hiyo hili nalo
Mheshimiwa Rais kama nalo unaweza kwenda kuliangalia nitashukuru sana,”
amesema.
Akijibu
hilo katika hotuba yake, Rais Samia amesema uwezekano uliopo ni kupunguza tozo
hiyo, lakini si kuiondoa kabisa.
“Ni kweli
Daraja la Kigamboni tunatoa tozo lakini hii imetokana na mradi wenyewe
ulivyojengwa. Daraja la Kigamboni ni mkopo na kama ni mkopo lazima tuurudishe
na hakuna wa kurudisha zaidi ya sisi wenyewe wananchi ni uzoefu wa kwanza kuona
wananchi wanalipa kupita pale,” amesema.
Ameeleza
baadhi wanafananisha mradi huo na Daraja la Tanzanite, akifafanua kinachotozwa
kwenye mradi wa Julius Nyerere kinatokana na deni lililopo, wakati daraja la
Tanzanite limejengwa kwa fedha ya Serikali.
“Wengine
walisema mbona daraja la Tanzanite watu hawalipishwi, Tanzanite ni fedha ya
Serikali asilimia 100, daraja la Kigamboni ni mkopo lazima urudishwe, lakini
nataka niseme wananchi sasa mzoee huduma za namna hii na barabara za namna hii
zitakuja nyingi.
“Ile kila
kitu bure kidogo kidogo itakuwa inaondoka, ili tuiendelee lazima tuwe na
barabra, madaraja na vivuko vizuri na hayo yataletwa na sekta binafsi ili
iendelee lazima tulipie hiyo huduma, kwa hiyo tozo tunaweza kuangalia kuipunguza
lakini sio kwa kuiondosha,” Rais Samia.
0 Comments