Header Ads Widget

MVIWATA WATAKA WAWEKEZAJI WAWEKEZE VIWANDANI MASHAMBANI WAWAACHIE WAKULIMA


 Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE

Wakulima mkoani Njombe wameshauri wawekezaji waachane na biashara ya kuwekeza mashambani na badala yake wawekeze kwenye viwanda vitakavyowasaidia wao kupeleka mazao yao.


Katika mkutano mkuu wa mtandao wa vikundi vya wakulima MVIWATA Tanzania  katika mikoa ya Njombe na Iringa baadhi ya wanachama hao ambao ni wakulima wanasema kitendo cha wawekezaji kwenda kuwekeza mashambani kinawanyima fursa wakulima ambao ndio wahusika wakuu katika sekta ya kilimo.


Hosea Mangula,Sikujua Mbata,John Kiswaga na  Sarah kaduma ni baadhi ya wakulima wanaosema wawekezaji wanaoingia mashambani kuwekeza pia wanasababisha kuibuka kwa migogoro ya ardhi inayochochea chuki baina ya wakulima, Wawekezaji na serikali inayowaruhusu wawekezaji hao kuingia kwenye sekta ya Kilimo.


Mjumbe mteule wa bodi ya  MVIWATA taifa Veronica Soph amesema wakulima sasa wanaweza kulima kwa tija na hivyo Serikali iwekeze kwa wakulima wadogo ambao wakiungana wanaweza kuongeza kiwango Cha uzalishaji.


Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka ametumia fursa hiyo  kuwataka wataalamu wa kilimo kuwatembelea wakulima mashambani na kuwapa elimu ya kilimo bora badala ya kufikiria kukusanya ushuru wa mazao pekee.


Aidha Mtaka amesema ni lazima sasa kuwapo kwa utaratibu wa serikali kuwatambua wakulima bora ndani ya mkoa ili kuwapa hamasa wakulima wengine kwenda kuzalisha kwa tija.









Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS