Header Ads Widget

ASKARI WATANO MBARONI KWA KUSAFIRISHA WAHAMIAJI HARAMU MBEYA.


     Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia Askari Polisi wa Tano kwa tuhuma za kusafirisha wahamiaji haramu 6 raia wa Ethiopia Kuelekea Wilayani Kyela Mkoani humo Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishina msaidizi wa Polisi Benjamin Kuzaga, amesema Askari hao wamekamatwa October 20 katika kituo kidogo Cha Polisi Uyole, wakiwa na wahamiaji 6 kwenye gari yenye namba T 946 BTT mali ya Polisi F.8497 CPL Simon Billia. Kuzaga amewataja Askari hao wanaoshikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kuwa ni ASP. Thomas Bwile, F.3132 SGT Beda Moriss, F.8497 CPL Simon Billia, G.3146 CPL Mohamed Ndungulu na G.6364 CPL Joseph Manumbu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI