Header Ads Widget

KOROSHO KILO 1,658,990 ZIMEUZWA PWANI

 


Na Scolastica Msewa, Kibiti.

Kilo 1,658,990 za korosho zimeuzwa baada ya wakulima kuridhia bei ya wastani ya shilingi 1675 katika mnada wa kwanza wa korosho wa mkoa wa Pwani uliofanyika Wilayani Kibiti mkoani pwani.


Akitoa taarifa kwenye mnada huo Meneja wa Chama kikuu cha Ushirika wa Wakulima mkoa wa Pwani CORECU Mantawela Hamisi katika mnada huo uliohusisha Wadau mbalimbali wa Vyama vya Msingi vya wakulima wa Mkoa huo na uongozi wa Wilaya ambapo Mkuu wa Wilaya ya Kibiti ambaye ni Kaimu Meja Edward Gowele akiwa Mwangalizi wa Mnada huo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge.


Alisema mnada huo umewakilisha korosho zote zilizokusanywa katika maghala ya wilaya zote saba za mkoa wa Pwani ambapo bei hiyo iliyopatikana ni kutokana na kuchukua bei ya wastani zilizoombwa na wanunuzi katika sanduku la maombi ya wanunuzi wa korosho msimu huu.


Alisema “bei ya shilingi 1621.24 ilikuwa ni bei ya kiwango cha chini bei ya wanunuzi kilichoombwa katika mnada huo huku bei ya juu ilikuwa ni shilingi 1675 ikifuatiwa na bei ya shilingi 1650 ambapo kwa kuchukua bei ya wastani iliyoombwa na kuchakatwa ikapitishwa bei hiyo ya shilingi 1675” 


Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Meja Gowele aliwahimiza wasimamizi wa ukusanyaji wa Korosho kusimamia ubora na viwango vya daraja la kwanza la zao hilo na sio kukwamisha upatikanaji wa daraja hilo kwa kusababisha kukusanya Korosho za daraja la chini nyingi na kurudisha nyuma nafasi ya ubora wa korosho za mkoa huo.


“Tunahitaji tupande juu ya tulipoishia mwaka jana na hili jukumu ni letu sote yaani sisi wakusanyaji na wakulima wetu kwani hii itatusaidia kukuza uchumi wetu” alisema Meja Gowele.


Aidha aliwataka viongozi wa wakirishi wa vyama hivyo vya wakulima wa Mkoa wa Pwani kutumia vizuri nafasi hiyo kwa kujadiliana kwa pamoja na kufikia muafaka wa uuzaji wa korosho zao.


Kaimu Mwenyekiti wa CORECU Dollar Chaurembo aliomba uongozi wa bodi ya korosho Tanzania kuhakikisha wahudhuriaji wa mikutano ya Bodi hiyo inahudhuriwa na wakulima wenyewe wengi na sio kama ilivyokuwa katika mikutano iliyopita ambapo wakulima uhudhuria wachache kwa kuwakirishwa na viongozi ambao hawajui changamoto wanayokutana nayo wakulima shambani.


Naye Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na ubora wa Bodi ya Korosho Tanzania Domina Mkangara alisema bodi hiyo kwa sasa ipo katika utafiti wa jinsi ya kuongeza thamani kwenye mnyororo wa zao la korosho kwa sababu ya kutafuta namna ya kusindika korosho ili isafirishwe nje ya nchi ikiwa imebanguliwa.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS