Header Ads Widget

KILO MILIONI 4.77 ZIMEUZWA KWENYE MNADA WA SITA RUNALI

 

NA HADIJA OMARY, LINDI

JUMLA ya kilo milioni 4.77 za korosho ghafi za chama kikuu cha ushirika RUNALI kinachojumuisha wakulima wa Wilaya za Ruangwa, Nachingwea na Liwale Mkoani Lindi zimeuzwa katika mnada wa sita wa chama hicho kwa bei ya juu ya shilingi 1985 na bei ya chini 1960.


Mnada huo umefanyika katika Kijiji cha Mikunya Wilayani Liwale Mkoani Lindi ambapo jumla ya makampuni 21 yaliomba kununua korosho hizo huku mahitaji yakiwa kilo milioni 10.73.


Akizungumza baada ya kumalizika kwa mnada huo makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Mikidadi Mbute aliwataka watendaji wa Chama hiko cha RUNALI kuendelea kufanya michakato ya malipo mapema ili wakulima walipwe fedha zao kwa wakati.


Alisema chama hicho kinakila sababu kuharakisha malipo kwa wakulima kwa kuwa mkulima anapolima mazao yake na kukusanya anatarajia kuuza na kupata fedha yake kwa wakati


“ hii ni kwa sababu wapo wakulima wanasomesha Watoto, ukiacha kusomesha mwaka huu imeonekana kwamba kwenye Nchi yetu kuna dalili ya njaa wakulima watanunua akiba ya chakula pamoja na kuandalia mashamba kwa ajili ya msimu wa ufuta kwa mwaka” alisema Mbute

 

Kwa upande wake Mhasibu Mkuu wa Chama kikuu cha Ushirika RUNALI Hashimu Abdala aliwahakikishia wakulima wanaohudumiwa na chama hicho kulipwa fedha zao kwa wakati ndani ya wiki moja baada ya mnada kufanyika ili mkulima aweze kujikimu mahitaji yake ya msingi na ya kimaendeleo

 

Naye mrajisi wa vyama vya ushirika Mkoani Lindi Secilia Sostenes alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa wakulima wa Mkoa huo wasio wanachama kujiunga kwenye vyama vya ushirika ili kuimarisha vyama hivyo

 

Secilia alisema Vyama vya ushirika vimekuwa msaada mkubwa kwa jamii ya Tanzania na Zaidi katika mikoa ya kusini ambayo inalima korosho na ufuta ambapo wakulima uuza mazao yao kupitia vyama vya ushirika.

 

Aidha aliongeza kuwa Vyama hivyo vya ushirika licha ya kuwahudumia wanachama lakini pia vinahudumia wakulima wasio  wanachama hivyo ili kuunganisha sauti ya pamoja ni muhimu kwa wakulima ambao sio wanachama kujiunga katika vyama hivyo.






Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI