Jamii ya kifugaji ya kimaasai imetakiwa kuepuka kuwapeleka watoto wao machungani kuchunga ng'ombe na badala yake wawapatie elimu itakayowasaidia katika kujikwamua kiuchumi na kujitegemea katika maisha Yao.
Akizungumza katika Mahafali ya chuo Cha viwanda na misitu FITI, Oloibok Lekisamba kutoka wilaya ya monduli ambaye ni mzazi wa aliyehitimu katika Ngazi ya Stashahada ya teknoloJia ya viwanda vya misitu na kufaulu na kuwa Mwanafunzi Bora kwa miaka mitatu mfululizo katika chuo hicho.
Amesema kuwa anamshukuru Mwenyenzi Mungu kwa Lazaro kufanya vizuri na kuonesha mfano mzuri katika chuo hicho.
Aidha amesema kuwa yeye Kama mzazi aliona ni vyema kumsomesha mtoto wake huyo kwani elimu ndio kitu pekee na itakayomsaidia kujua kinachoendelea na kusema kuwa kumzuia mtoto kwenda shule ili aende kuchunga ng'ombe pamoja na kumrithisha ng'ombe inakuwa haina faida Bali ni hasara kwani ng'ombe wanaweza kupata madhara na hata kufa hususani katika kipindi Cha kiangazi.
Hata hivyo amesema mbali na kuwepo kwa changamoto ya ukosefu wa pesa za kulipia ada Bado aliweza kupambana na kumlipa ada ili aweze kutimiza ndoto zake za kuhitimu mafunzo.
Kwa upanda wake Lazaro Oloboku amesema Kuwa anamshukuru Mwenyezi Mungu pamoja na wazazi kwani kufanya kwake vizuri imechangiwa na wazazi ambao wamejitahidi kumshauri na kumlipia ada kwa wakati.
Pia amewataka wazazi hususani wa jamii ya kimaasai kuwapeleka watoto wao shuleni na sio kuwazuia ili waende machungani kuchunga ng'ombe Bali wawapeleke shuleni kwani elimu ni nzuri na pia itawasaidia kwenda viwango vya juu.
Hata hivyo amewataka vijana kujiajiri wenyewe kwani kukaa majumbani na kusubiri ajira Serikali inapoteza muda .
Ameiomba Serikali kuipatia vyuo vya kati mikopo kwani Kuna changamoto ya wanafunzi wengi kukosa pesa za kulipia ada na kusema Kama mikopo ikitolewa itachangia kupunguza tatizo Hilo.
0 Comments