Header Ads Widget

DC , RUANGWA ASIKITISHWA NA WAZAZI KURUHUSU WATOTO KUCHOMWA SINDANO KUZUIA UJAUZITO

 


NA HADIJA OMARY _LINDI.


Wasichana wanaoishi Mikoa ya Lindi na Mtwara wapo hatarini  kukumbwa na tatizo la utasa, kutokana na baadhi ya wazazi kulazimisha watoto wao wa kike,matumizi ya kuchomwa Sindano za kinga kuzuia kupata Mimba wakiwa na umri mdogo.



Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Hassani Ngoma, wakati anazungumza na vijana kwenye Mdahalo wa kujadili changamoto zinazowakabiri vijana,wakiwemo walioathirika na virus vya VVU katika maadhimisho wiki ya siku ya Ukimwi Duniani,yanayofanyika Kitaifa Mkoani Lindi.



Akizungumza kwenye mdahalo huo,amesema maambukizi  mapya ya VVU yanayoendelea kuongezeka hivi sasa,yanatokana na kundi la vijana wa kiume na wa kike kutokuwa na hofu ya kumuogopa Munguna kubeza matumizi ya Zana (Kondomu) wakati wanatekeleza majukumu yao ya kistarehe.





Ngoma ametaja mambo mengine yanayosukumua kuongezeka kwa tatizo hilo,ni pamoja na kushamili kwa matumizi ya Sindano za kuzuia upatikanaji wa Mimba,unaoendelea kutolewa maeneo mbalimbali ya vituo vya kutolea huduma za Afya na Maduka ya kuuza Dawa muhimu.



Amesema katika Wilaya anayoiongoza watoto wa kike walio na umri kuanzia miaka nane hadi 13 wanachomwa sindano za kuzuia wasipate ujauzito,huku wazazi wakidaiwa kuweka msisitizo wa vijana wao kuchomwa sindano za aina hiyo,jambo alilodai sio sahihi na hatari ya kupata maambukizi ya VVU na ugumba.




“Watoto wa kike hivi sasa hawahitaji matumizi ya Kondomu,kutokana na matumizi ya sindano ya kuzuia kupata ujauzito”Alisema Ngoma.




Mkuu huyo wa Wilaya amesema hali hiyo isipodhibitiwa kuna hatari ya kuongezeka kwa maambukizi ya Ukimwi,huku kiwango cha kuzaliana watoto kwa upande wa kanda ya kusini kwa Mkoa ya Lindi na Mtwara ikashuka.


Amesema kutokana na hali hiyo, baadhi ya Shule zikiwemo za msingi ndani ya Wilaya ya Ruangwa kutoongezeka,huku akieleza zipo baadhi zina wanafunzi (126) kiwango alichokitaja ni kidogo ikilinganishwa na maeneo mengine.


“Baadhi ya Shule wanafunzi wanaomaliza Elimu ya darasa la saba ni kati ya saba au nane kutokana na kushiriki zaidi mapenzi kuliko masomo” Alisema Ngoma.


Mkuu huyo wa Wilaya ya Ruangwa amesema tatizo hilo,lisipodhibitiwa ni hatari ya kuongezeka kwa maambukizi ya virus vya ugonjwa wa Ukimwi na wanawake kupata tatizo la ugumba kutokuwa na watoto, hivyo kunaweza kuiweka kusini na Taifa kwa ujumla katika mazingira magumu.


Awali akieleze hali ya viwango vya maambukizi ya Ukimwi kwenye mdahalo huo,Mkurugenzi wa Taifa kudhibiti Ukimwi nchini (TACAIDS) Dr Leonard Maboko alisema maambukizi yameendelea kupungua na yaliyopo kwa hivi sasa idadi kubwa ipo kwa vijana kwa asilimia 30% wakati washana ni asilimia 80%.



 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI