Header Ads Widget

DC NANYUMBU APONGEZA UJENZI WA ZAHANATI YA KIJIJI NANDERU

 


Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Mariam Chaurembo amewahamasisha wananchi wa Kijiji cha Nanderu, Kata ya Nanyumbu kujitolea katika ujenzi wa Zahanati Chitowe ikiwa ni sehemu ya serikali kuboresha huduma za afya Wilayani humo. 


Kauli hiyo ameitoa wakati akishikiri ujenzi wa zahanati hiyo ambayo ni ya Kijiji na itawaasaidia wananchi wengi kuepukana na adha wanayokutana nayo. 


Katika eneo hilo Mkuu huyo  ameshirikiana na  Wananchi katika  kubeba  matofali na kujaza kifusi katika Zahanati hiyo inayojengwa. 


"Mmefanyakazi kubwa nawapongeza kwa kusaidia uboreshaji wa sekta ya elimu na afya tunaona juhudi kubwa zinazofanywa na wananchi nawaahidi serikali itamalizia zahanati hii"



Serikali inawajibu wa kuhakikisha kuwa  ifikapo Mwakani Zahanati hii itoe huduma kwa Wananchi  na wakazi wa kijiji cha Nanderu kwani umbali wa kutoka hapa mpaka kilipo kituo cha  Afya ni mrefu sana"


"Sio tu kwenye uboreshaji wa afya na elimu pia mmefanya vizuri katika matokeo yenu pongezi kwa Walimu wa Shule ya Msingi Nanderu kwa kufanya vizuri katika kuhakikisha Watoto/Wanafunzi wanakuwa na Uelewa wa kutosha hususani katika kuzifahamu KKK"




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS