Header Ads Widget

BOISAFI NA MFINANGA WAIBUKA KIDEDEA UCHAGUZI WA CCM MKOA WA KILIMANJARO.

 



Na WILLIUM PAUL, MOSHI.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro, Patrick Boisafi ameweza kutetea nafasi yake kwa kupata kura 881 na kuwaangusha Alphonce Temba (26) na Golden Swai(32).



Uchaguzi huo uliofanyika leo katika ukumbi wa CCM mkoa wa Kilimanjaro ambapo Msimamizi wa uchaguzi huo ni Mkuu wa mkoa wa Tanga, Omary Mgumba.



Akitangaza matokeo hayo, Mgumba aliwataka wanachama walioshinda kuvunja makundi ndaniya chama na kuwaunganisha wanachama na kuwa wamoja.



Katika nafasi ya Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi kupitia mkoa wa Kilimanjaro, Seleman Mfinanga ametetea nafasi yake kwa kupata kura 862 akiwabwaga Tumaini Mushi na Yusuph Furutuni.


Mwisho..

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI