Header Ads Widget

WAZIRI MKUU ARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI WA MABEHEWA YA SGR

 


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa katika ziara ya kikazi nchini Korea ametembelea kiwanda cha cha kampuni ya Sung Shin Rolling na kuona maendeleo ya utengenezaji wa mabehewa ya Reli ya Kisasa (SGR) ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) ambayo yanatengenezwa katika kiwanda hicho. 



Viongozi wengine waliotembelea kiwanda hicho ni pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Korea, Togolani  Mvura, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Balozi Mbarouk Mabarouk,  Rais na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Sung Shin Roliing, Gye Shul Park na kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Emmanuel Tutuba.


                                XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ameridhishwa na maendeleo na kasi ya ujenzi wa mabehewa mapya kwa ajili Reli ya Kisasa (SGR) ya Shirika la Reli Tanzania yanayotengenezwa na kampuni ya Sung Shin Rolling Stock (SSRT) iliyoko nchini Korea Kusini.


"Kati ya mabehewa 81 ambayo Tanzania inatengeneza kutoka kwenu, tayari 36 yamekamilika na yameshapelekwa nchini Tanzania na 45 yaliyobaki yanategemewa kukamilika Machi, 2023. Mabehewa haya ni ya daraja la tatu na yatatoa huduma zote muhimu."


Mheshimiwa Majaliwa ameyasema hayo mara baada ya kutembelea kampuni ya SSRST inayotengeneza mabehewa na injini za treni nchini Korea Kusini.


Kadhalika, Waziri Mkuu amemkaribisha nchini Rais wa Kampuni hiyo Gye Shul Park aje kuwekeza nchini Tanzania kutokana na fursa mbalimbali zilizopo ikiwemo mpango wa Serikali wa kuendelea kuiboresha sekta ya usafiri wa reli.


"Mnakiwanda kikubwa, teknolojia ya hali ya juu pamoja na utaalamu na watalaam kwenye eneo hili. Kwa sasa tuna mipango mikubwa ya kuendelea kuiboresha sekta hii ya usafiri wa reli, yapo maeneo tofauti kwenye mpango wa kuunganishwa na reli ya kisasa (SGR), nakukaribisha kuja kuwekeza kitu kama hiki Tanzania.


Aidha, Mheshimiwa Majaliwa alitembelea kituo cha Seamul Undong ambacho ni taswira ya maendeleo ya Korea kupitia mpango wa kuviwezesha vijiji ambao unatekeleza mpango huo nchini Tanzania katika mkoa wa Morogoro (Pangawe) na Zanzibar.


Mheshimiwa Majaliwa alimshukuru Rais wa Kituo hicho na kumuomba kuendelea kutoa ushirikiano ili kukuza zaidi mpango huo na kufikia maeneo mengi zaidi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS