Header Ads Widget

KIGOMA YAWEKA MKAKATI WATU WOTE KUPATA CHANJO YA UVIKO 19

Mkuu wa mkoa Kigoma Thobias Andengenye (katikati aliyesimama)  akizungumza katika kikao cha kamati ya afya ya msingi ya mkoa
Mganga Mkuu wa mkoa Kigoma Dk.Jesca Lebba (kushoto) akitoa maelezo kuhusu chanjo za UVIKO na Ebola kwa kamati ya afya ya msingi ya mkoa
Wajumbe wa kamati ya afya ya msingi ya mkoa wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa

                                        XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

 MKOA Kigoma umeanza kutekeleza mpango wa kutoa chanjo ya UVIKO 19 kwa watu wote ambao hawajapata chanjo hiyo ili kuhakikisha watu wote mkoani humo wanapata chanjo.


Mganga Mkuu wa mkoa Kigoma,Dk.Jesca Lebba alisema hayo akitoa taarifa kwa Mkuu wa mkoa Kigoma wakati wa kikao cha wajumbe wa kamati ya afya ya msingi ya mkoa kueleza mikakati ya kukabiliana na ugonjwa wa Ebola na chanjo.


Alisema kuwa katika kampeni hii ya sasa wanatarajia kuwapa chanjo watu 110,458 ili kufikia lengo la kuchanja watu 1,375,732 idadi ambayo itafanya watu wote mkoani humo kufikiwa.


“Kampeni hii ya sasa iliyoanza Oktoba 17 mwaka huu itahitimishwa Oktoba 30 ambapo njia mbalimbali zitafikiwa ikiwepo kuwepo kwa vituo 256 vinavyotoa chanjo hiyo lakini pia njia ya utoaji chanjo kwa watu wanaotembea (Mkoba) itafanyika ili kuwafuata watu walipo,”Alisema Mganga huyo Mkuu wa mkoa Kigoma.


Mganga huyo Mkuu wa mkoa alisema kuwa kwa sasa mkoa una chanjo 70,130 za Jensen, dozi 124,423 za Sinopham na dozi 12,970 za Sinovac na tayari chanjo hizo zote zimeshapelekwa kwenye vituo vinavyotoa chanjo.


Akizungumza katika kikao hicho Mkuu wa mkoa Kigoma, Thobias Andengenye aliwashukuru wajumbe wa kamati hiyo ya afya ya msingi hasa viongozi wa dini kwa kazi kubwa ya uhamasishaji waliyofanya na kuwataka kutumia nafasi hii ya sasa kuhamasishaji waumini watu wote kujitokeza kupata chanjo hiyo.


Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa takwimu na taarifa mbalimbali zinazotolewa na wataalam wa afya nchini zinaonyesha kuwa watu waliopata chanjo wamekuwa hawapati madhara wanapopata maambukizi ukilinganisha na wale ambao hawajapata chanjo jambo linaloonyesha umuhimu wa chanjo hiyo.


Baadhi ya wajumbe waliohudhuria kikao hicho akiwemo Mwenyekiti wa CCM mkoa Kigoma, Amandus nzamba alisema kuwa umasishaji umekuwa na mafanikio kwa mkoa Kigoma na wao kwa nafasi yao wataendelea kuhamasisha ili kufikia lengo la utoaji chanjo lililowekwa.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS