Header Ads Widget

WAZAZI MKOANI PWANI WATAKIWA KUACHA TABIA YA KUWAOZESHA WATOTO WA KIKE.

WAZAZI Mkoani Pwani wametakiwa waache tabia ya kuwaozesha watoto wao wa kike badala yake wawapatie elimu ili watimize ndoto zao.


Akizungumza kwenye mahafali ya shule ya Msingi ya Muungano katibu wa Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere Omary Pumzi alisema kuwa watoto wa kike wana ndoto zao za baadaye kama walivyo watoto wa kiume.


Pumzi alisema kuwa serikali haitasita kuchukua hatua kali kwa wazazi wanaowaozesha watoto wao badala ya kuwapatia elimu.


"Mtoto kupata elimu ni haki ya Msingi ambayo anatakiwa kuipata kama wanavyotoa kipaumbele kwa watoto wa kiume,"alisema Pumzi.


Alisema kuwa watoto wa kike ambao wazazi wao waliwapatia elimu wamepata mafanikio makubwa kama ilivyo kwa Rais Samia Suluhu Hassan na wengine wengi.


"Itashangaza kuona mzazi kachukua fedha mahari kwa ajili ya kumuoza mtoto wake kisa eti kamaliza darasa la saba   kwa aliyefanya hivyo ajiandae kuzirudisha kwani atakutana na mkono wa sheria,"alisema Pumzi.


Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Faith Thawe alisema kuwa changamoto kubwa ni shule hiyo kukosa uzio hali inayosababisha wizi wa mali za shule.


Kwa upande wake Mariam Mbinda akisoma risala ya wahitimu alisema kuwa upungufu wa vyoo 33 vya wanafunzi ni changamoto kubwa sana kwani vilivyopo ni nane tu wanafunzi 79 walitunukiwa vyeti vya kuhitimu masomo ya elimu ya Msingi.  


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI