Header Ads Widget

MWENYEKITI UVCCM MOSHI VIJIJINI AWAFUNDA WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE

 


Mwandishi wetu, Moshi.


Wanafunzi wa kidato cha nne kutoka shule ya sekondari Himo, Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, wameaswa kutoridhika na kiwango cha elimu walichofikia kwani huo ndio mwanzo wa  kuzifikia ndoto zao za kitaaluma.


Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Umoja wa vijana wa chama cha Mspinduzi, (UVCCM) Wilaya ya Moshi vijijini, Yuvenal Shirima wakati akizungumza na wanafunzi hao kwenye mahafali ya 16 ya kidato cha nne shuleni hapo.


"Niwapongeze wahitimu kwa kujitoa kwenu na kuzingatia  masomo hadi kufikia hatua ya  kufanya Mahafali haya, niwasihi mjiandae vyema na Mitihan ya Taifa ilioko mbele yenu kwani hapa mlipo ndiyo mwanzo wenu wa kuzifikia ndoto zenu kimaisha"amesema Shirima


Amesema katika kuyafikia mafanikio ya kimaisha ni lazima wasome kwa bidii ili waweze kufaulu katika mitihani yao ya mwisho na kuendelea na hatua nyingine za kielimu, ambapo pia amewaasa wazazi kuwalea watoto katika misingi iliyo bora, ikiwa ni pamoja na kuepuka kuwafanyia vitendo vya kikatili.


"Lakini pia niwakumbushe wazazi kuwaunga mkono watoto wenu kama mlivyofanya hadi kuwawezesha kufikia hapa, ili waweze kufanya mitihani pasipo vikwazo vyovyote toka kwa wazazi na walezi, na niwaombe epukeni kutoa maneno makali kwa watoto wenu au kuwafanyia vitendo vya kikatili, kwani kufanya hivyo ni kukatisha ndoto zao za baadae na wengine kuwafanya kuwa tegemezi".


Aidha Mwenyekiti huyo ambaye ameahidi kurekebisha Darasa Moja kwa kulifanyia ukarabati na  Kutoa printer moja shuleni hapo, pia  amempongeza Rais na Mwenyekiti wa CCM Samia Suluhu Hasani kwa kazi nzuri anayofanya ikiwemo kuwezesha kujengwa madrasa manne katika shule hiyo. 


Akitoa taarifa ya Shule, mkuu wa shule hiyo, Zablon Mhadisa amesema wanakabiliwa na changamoto mbalimbali, ikiwemo uhaba wa maabara moja 


uchakavu wa miundombinu ya madarasa matano, pamoja na uhaba wa vifaa vya maktaba.



Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI