Header Ads Widget

WAWEKEZAJI WAZAWA WAIOMBA SERIKALI KUBORESHEWA HUDUMA YA UMEME KUPUNGUZA GHARAMA YA UZALISHAJI

 


Teddy Kilanga Arusha 

Wawekezaji wazawa wameiomba serikali kuboresha huduma ya umeme na kuweka mkakati wa kudumu ili kupunguza gharama ya uendeshaji kutokana na mgao wa huduma hiyo inapokata.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelewa na watendaji wa kiwanda kidogo ,Meneja wa kiwanda cha bia mkoa wa Arusha,(TBL)Joseph Mwaikasu alisema mgao wa huduma ya umeme inayoendelea kwa sasa inawagharimu hasa katika upande wa uendeshaji hivyo wanaiomba serikali kupitia shirika la nishati ya umeme Tanzania(Tanesco) kuboresha huduma hiyo.

"Changamoto ya mgao wa umeme kwa sasa inatugharimu kwa kiasi kikubwa kwani tunatumia jenereta ukiangalia mafuta ya dizeli pia yapo juu hivyo tunaiomba serikali itusaidia kuweka mikakati ya kudumu ili kupunguza adha hii,"alisema Mwaikasu.

Sambamba na hilo Mwaikasu alisema kuwa  huwa wanawapatia ujuzi watendaji wa viwanda vidogo ili wajifunze juu uendeshaji kwa lengo la kufikia viwango vya kimataifa na kuweza kuajiri vijana wengi zaidi nakueweza kupunguza changamoto za ajira nchini.

"Kwa upande wa kiwanda chetu tumefanikiwa kuajiri vijana takribani 150 hivyo bado tunaendelea kutumia fursa za ajiri watu mbalimbali lengo ni kila mmoja aweze kunufaika na uwekezaji wa kiwanda hiki ,"alisema.



Saphira Von Moos, Ofisa Mkuu Uendeshaji (COO) kutoka Kampuni ya Bia ya Twiga ametoa sababu kadhaa kwa nini wamechagua TBL na si kampuni nyingine yoyote katika kupata ujuzi na uzoefu mpya katika kufikia malengo yao kama kampuni mpya ya kutengeneza bia.

"Tumechagua TBL kwa sababu ni moja kati ya kampuni kubwa nchini Tanzania haswa katika tasnia ya bia na wana uzoefu mkubwa, ujuzi na utendaji bora ambao tungependa kuwapa timu yetu na kufanya kazi pamoja na kanuni ambazo tumejifunza. leo ili tufikie malengo yetu kadri tunavyozidi kukua".

Saphira aliongeza kuwa makampuni yote yanaanza na kanuni ambazo zinafanya kazi pamoja ili kuweka malengo na kuyasaidia kukua hivyo TBL imewasaidia kuona umuhimu wa kuwa na kanuni zitakazowaongoza katika kufikia malengo yao na kukua kwanza iwezekanavyo. 

.zaidi Saphira alisema kupitia mafunzo waliyopata leo yamewasaidia kuona umuhimu wa kuhifadhi mazingira na bidhaa wanazozalisha kwa kufanya kazi na watu na mazingira yao.

"Ni muhimu kwetu kujua umuhimu wa kuweka mazingira salama kwa lengo letu ni kuwa na bidhaa bora na zenye ubora, kama huna mazingira mazuri ya uzalishaji hutakuwa na bidhaa bora zinazohitajika sokoni".

kufanya kazi pamoja na kushirikisha kila mtu katika uzalishaji ndio huleta matokeo chanya ya bidhaa, hiki ndicho wanachofanya TBL ndiyo maana wanakuwa na matokeo chanya kwa kila wanachofanya na kuzalisha" Von Moos aliongeza.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI