Header Ads Widget

WATUMISHI 139 WAFADHILIWA MASOMO NDANI NA NJE YA NCHI

 


Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma


JUMLA ya Watumishi 139 wamechaguliwa kupata ufadhili wa masomo kwa Set katika fani ya ubingwa na ubingwa bobezi huku kati ya hao, Watumishi 136 watasomeshwa nje ya nchi na Watumishi 3 watasomeshwa ndani ya nchi .


Hayo yamesemwa leo Jijini hapa na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu wakati akitoa taarifa kuhusu mpango wa Serikali wa kuendeleza Watumishi wa Sekta ya Afya katika fani za ubingwa na ubingwa bobezi nchini.


Waziri ummy amesema, Mpango umepewa jina la "Mpango wa Samia wa kuongeza Wataalamu Bingwa na Bobezi wa Afya nchini " utakao gharimu shilingi Bilioni 8.


Aidha, Waziri Ummy amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, kwa kukubali kuongeza fedha kiasi cha Shilingi Bilioni 8 zitakazotumika kugharamia wataalamu waliochaguliwa kusoma mafunzo haya.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI