Header Ads Widget

WALIMU SONGEA WATAKIWA KUTOKUACHA KADI ZAO ZA BENKI KWA WATU WANAOKOPESHA FEDHA MITAANI.

 




Na Amon Mtega, Songea.



AFISA Elimu Vifaa na takwimu Elimu ya Msingi Songea Vijijini Mkoani Ruvuma Daniel Ngongi amewataka Walimu kuacha tabia ya kukabidhi kadi zao za benki wanazochukulia mishahara kwa watu wanaokopesha fedha mitaani ili kulinda siri ya mishahara yao.


 Ngongi ametoa wito huo wakati akizungumza kwenye mkutano mkuu wa miaka miwili na nusu wa Chama cha Walimu CWT Wilaya ya Songea Vijijini yenye Halmashauri mbili ya Songea na Halmashauri ya Madaba.

 


 Afisa Elimu huyo ambaye amemwakilisha mkurugenzi wa Halmashauri ya Songea Neema Maghembe kwenye nafasi ya ugeni rasmi kwenye mkutano huo amesema kuwa kumekuwepo kwa baadhi ya Walimu wamekuwa wakiacha kadi za benki kwa  watu wanaokopesha fedha jambo ambalo limekuwa likiwaondolea heshima na kuwafanya kusiwepo na usiri wa mishahara yao.


Aidha Ngongi akizungumzia baadhi ya changamoto zinazowakabili Walimu kufuatia risala ambayo imesomwa na katibu wa CWT Songea Vijijini Adriano Ngailo amesema kuwa changamoto nyingi tayari zimeanza kufanyiwa kazi ikiwemo za malimbikizo ya madai mbalimbali yakiwemo ya matibu kwa watumishi na kuwa changamoto nyingine kama za makosa kwenye usimamizi wa mitihani na usimamizi wa majengo ya shule (Madarasa)nijambo linalohusisha taasisi mbalimbali za kisheria hivyo zitajadiliwa na mamlaka husika.




Kwa upande wake katibu wa CWT Songea Vijijini Adriano Ngailo awali akisoma risala amesema kuwa  Walimu waliowengi bado hawajalipwa fedha za matibu licha ya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuonyesha nia ya kuyalipa madeni hayo jambo ambalo Walimu wanaonyesha kuwa na imani na Serikali yao.


 Akizitaja changamoto zingine kuwa kumekuwepo kwa baadhi ya Walimu kuogopa kufanya kazi za Kiserikali kama kusimamia mitihani na ujenzi wa majengo ya shule (Madarasa)kuwa kumekuwepo kutokuwa na Lugha za ushirikiano zaidi ya vitisho pindi panapohisiwa kuwa kunachangamoto zimejitoleza kwenye kazi hizo.



Katibu huyo amefafanua kuwa kwenye changamoto za kusimamia mitihani ambazo inawezekana mwalimu amekuwa hazijui anaambiwa na mwajili Lugha ya mkusanye yeye na mitihani wapelekwe ofisi husika (Vyombo vya Dola)huku kwenye usimamizi wa majengo utakuta mwalimu hajapatia mchanganuo wa gharama za mradi (BOQ) anaambiwa atoe fedha za mshahara wake jambo ambalo limewafanya baadhi ya Walimu kukwepa kufanya kazi za Serikali.


Ngailo akisoma risala hiyo mbele ya mgeni rasmi pamoja na Wajumbe wawakilishi zaidi ya 130 kutoka kwenye matawi yao ya kazi kwenye shule za Msingi na Sekondari amesema kuwa licha ya kuwepo kwa changamoto hiyo ya madeni ya matibu lakini Chama cha Walimu CWT Songea Vijijini kinaishukuru Serikali kwa kuendeleza Ujenzi wa madarasa ya kwenye shule mbalimbali , utoaji wa Elimu pasipo malipo,upandishaji wa madaraja kwa Walimu.



 Naye mwenyekiti CWT Songea Vijijini Fausta Mwingira amesema kuwa Chama cha Walimu kipo kwaajili ya kutetea maslai ya Walimu ili waweze kutendewa haki pindi wanapokuwa kwenye sehemu zao za kazi.


 Mwenyekiti huyo pia amewaomba Walimu kuendelea kujituma kufanya kazi kwani Serikali ambayo ndiyo mwajili inaendelea kutatua changamoto ambazo zipo na zimeainishwa kwenye risala.



 Pia katibu wa CWT Mkoa wa Ruvuma Onesmo Makwembe wakati akitoa salamu  amewataka Walimu hao  kutumia Benki ya mwalimu (MCB)ili waweze kupata mikopo yenye riba nafuu  ambayo inadaiwa ipo tofauti na Benki zingine.

 

   

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI