Mwenyekiti wa Shirikisho la Walimu Makada wa CCM Jackson Kadutu amesema, wameamua kufanya zoezi la uchangiaji wa damu ikiwa ni kumuunga mkono Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ili kusaidia Mama Wajawazito na Watoto katika changamoto ya uhaba wa damu kituoni hapo.
Naye Katibu wa Shirikisho la Walimu Makada wa CCM Devid Sulube amesema, kwa pamoja katika Shirikisho hilo wameweza kuchanga kiasi cha shilingi milioni mbili na kununua mahitaji mbalimbali kwa ajili ya kutoa msaada katika Kituo cha Afya Buzuruga kwa ajili ya Mama na Mtoto
Afisa Tarafa ya Ilemela Suzana Tulimanywa amewapongeza walimu Makada wa CCM kwa kufanya zoezi la kizalendo la uchangiaji damu pamoja na kutoa msaada wa vifaa mbalimbali kwa mama wajawazito na watoto huku akitoa rai kwa vyama vingine kuiga mfano huo.
0 Comments