WAFANYABIASHARA nchini wametakiwa kusajili biashara zao kabla hawajaanza biashara ili wafanye kazi kisheria.
Hayo yalisemwa Mjini Kibaha na Mwanasheria wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Anneth Mfinanga alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa maonyesho ya biashara na uwekezaji ya Mkoa wa Pwani.
Mfinanga alisema kuwa hiyo ni changamoto kwani baadhi wanaanza biashara bila ya kusajili biashara zao.
"Brela inafanya usajili wa biashara, alama za biashara, usajili wa kampuni, majina ya biashara na kusajili ubunifu ni vema kabla mtu hajaanza biashara ni vema wakasajili ili wawe kisheria,"alisema Mfinanga.
Alisema kupitia maonyesho hayo watu wameweza kufanya usajili na kupata vyeti vyao ambapo changamoto ni baadhi kutokuwa na uelewa hivyo kutosajili kama sheria inavyotaka.
"Tunawashauri wajisajili wawe huru katika kufanya shughuli zao za kibiashara kwani huo ndiyo utambulisho wa biashara zao,"alisema Mfinanga.
Aidha alisema kuwa usajili wa biashara na kampuni zao ili waweze kufanya biashara zao kisheria ili kuondokana na usumbufu.
0 Comments