Header Ads Widget

POSTA IRINGA NA NJOMBE WAWAKUMBUKA YATIMA SIKU YA POSTA DUNIANI


Meneja wa shirika la Posta mkoa wa Iringa na Njombe 
Bernansgar clemence Olomi akikabidhi misaada Kwa mkuu wa kituo Cha kulea watoto Yatima Cha Huruma Center Mchg Joyce Ngandango.
,............................................

KATIKA kuadhimisha siku ya Posta Duniani,Shirika la Posta Mkoani Iringa na Njombe limetoa msaada wa vyakula ,Sabuni ,mafuta na vitu mbali mbali Kwa kituo Cha kulea Yatima Cha Huruma Center  lengo likiwa ni kurudisha kwa jamii kile ambacho wanakipata.


Akizungumza Mara baada ya kukabidhi msaada huo jana Meneja Posta Iringa na Njombe, Bernansgar clemence Olomi alisema Kila mwaka Oktoba 9 ni siku ya Posta Duniani na wao wameamua kufanya hivyo ili kurudisha kwa jamii kile ambacho wanakipata.

Amesema Yatima ni watoto wa jamii nzima na Kila mmoja anaowajibu wa kuwasaidia  .

Hata hivyo alisema Shirika la Posta Kwa Sasa limefanya maboresho makubwa ya huduma mbali mbali na kuwa wakati wakiadhimisha siku ya Posta Duniani wanajivunia mafanikio makubwa.

“Huduma zetu siku hizi zimeboreshwa zimebadilika kutoka manual sasa hivi tunafanya mambo kidigital tuna mfumo mpya ambao tunautumia ambao unatuwezesha mteja yoyote hata akiwa nyumbani kwake anapata huduma pamoja na kununua vitu online,”amesema Olomi

Alisema wanaadhimisha siku ya Posta Duniani na kwa mwaka huu wamekabidhi msaada katika kituo chicho Cha Huruma Center ili kuwafariji watoto kituoni hapo.

“Kwa kweli kwetu ni fahari na faraja kubwa kurudisha kwa jamii kile ambacho wamekuwa wakichangia katika shirika hili la uuma wajibu Wetu kuendelea mkono jitihada za Serikali na wadau kama ninyi  katika kuwasaidia watoto Yatima "

Alisema wanaushukuru uongozi wa shirika kwa jitihada wanazoendelea nazo za katika mageuzi ndani ya shirika kwani kuna mabadiliko mengi yamejitokeza ya kiuboreshaji wa huduma Kwa wateja.

Mkuu wa kituo hicho Cha Huruma Center Mch Joyce Ngandango  mbali ya kuipongeza msaada huo alisema kuwa kituo hicho kilianzisha mwaka 1994  na Askofu Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Iringa Dkt Owdenburg Mdegela

Kuwa kituo hicho kinalea watoto wa makundi mbali mbali wakiwemo Yatima ,wanaotoka kwenye mazingira magumu na wale wanaofanyiwa vitendo vya ukatili .

Baadhi ya wafanyakazi wa shirika la Posta mkoa wa Iringa na Njombe wakiwa kituo Cha Kulea watoto Yatima Cha Huruma Center
Wafanyakazi Posta mkoa wa Iringa wakifuatilia historian ya kituo 
Wafanyakazi Posta Mkoa wa Iringa na Njombe wakiwa kituo Cha Kulea watoto Yatima Cha Huruma Center
Wafanyakazi Posta mkoa wa Iringa na Njombe wakifurahia siku ya Posta Duniani Kwa kulishana keki

Picha ya pamoja ya wafanyakazi Posta mkoa wa Iringa na Njombe 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI