Header Ads Widget

WAHITIMU WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA KUFUATA MAADILI

Kamishina wa Sera kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Fredrick Mwakibinga akizungumza katika mahafali ya 11 ya Wahitimu wa Mitihani ya Kitaaluma ya PSPTB na kuishauri bodi hiyo kuendelea kutoa huduma kupitia ofisini yake ya Mkoa wa Dar es Salaam na maeneo jirani licha ya kuhamia rasmi jijini Dodoma toka Septemba 30,2022 wakati wa mahafali hayo yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi PSPTB Jacob Kibona amesema mahafali hiyo ni ya 11 tangu kuanzishwa kwa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi 2007 na kueleza kuwa kwa mujibu wa sheria iliyoanzisha Bodi hiyo, matokeo yote ya mitihani ya kitaaluma ya PSPTB ni lazima yapitiwe na kuidhinishwa na bodi ya Wakurugenzi.

                                    Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB  Godfred Mbanyi




                                xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Na Fatma Ally Matukio Daima APP Dar es Salaam

 Wahitimu wa fani ya ugavi na ununuzi wametakiwa kufanya kazi kwa kufata maadili ya kitaaluma ili kulinda heshima ya fani hiyo na kuleta ufanisi katika matumizi ya rasirimali za Umma kwa manufaa ya Taifa kwa ujumla.


Kauli hiyo ameitoa jijini Dar es   Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB  Godfred Mbanyi katika mahafali ya 11 ya mtihani wa kitaaluma ya PSPTB ambapo amesema wanahitaji kuona Sekta binafsi zikue kwa kufanya biashara kubwa Ili ziweze kulipa kodi na nchi iweze kuendeleza shughuli za maendeleo katika jamii.


"Tunaposema maslahi aidha mkitumika sekta binafsi au sekta za Umma wote mnahitaji kufanya kazi kwa maadili, Tunahitaji kampuni binafsi zikue kwa kufanya biashara kubwa ili ziweze kulipa kodi na Nchi iweze kuendeleza shughuli za maendeleo katika jamii." amesema Mbanyi.


Kwa upande wake, Kamishna wa Sera wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB,) Fredrick Mwakibinga ameishauri bodi hiyo kuendelea kutoa huduma kwa wateja wao kupitia ofisi ya Mkoa wa Dar es Salaam inayohudumia na maeneo yanayozunguka licha ya kuhamia rasmi makao makuu ya Nchi Dodoma.


"Napenda kuwapongeza wahitimu wote ambao mtatunukiwa vyeti pamoja na shahada za umahiri ila mfahamu kazi kubwa mnayokwenda kuifanya kwa jamii, ninaelewa vizuri hatua na changamoto mlizopitia leo mnastahili pongezi, jitihada zinazofanywa na bodi zinaonekana dhahiri endeleeni kuwahudumia watanzania katika ofisi za hapa Dar es Salaam na Dodoma pia " amesema Mwakibinga.


Naye, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi PSPTB Jacob Kibona amesema mahafali hiyo ni ya 11 tangu kuanzishwa kwa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi 2007 na kueleza kuwa kwa mujibu wa sheria iliyoanzisha Bodi hiyo, matokeo yote ya mitihani ya kitaaluma ya PSPTB ni lazima yapitiwe na kuidhinishwa na bodi ya Wakurugenzi.


"Kwa bahati mbaya kuanzia septemba 2019 hadi novemba 2021 PSPTB haikuwa na bodi ya wakurugenzi baada ya iliyokuwepo awali kumaliza muda wake hali hii ilipelekea kutokufanyika kwa mahafali kwa miaka mitatu napenda kuchukua nafasi hii kuishukuru Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango hatimaye bodi ya wakurugenzi imeteuliwa Novemba 2021." amesema Kibona.


Kamishina wa Sera kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Fredrick Mwakibinga akizungumza katika mahafali ya 11 ya Wahitimu wa Mitihani ya Kitaaluma ya PSPTB na kuishauri bodi hiyo kuendelea kutoa huduma kupitia ofisini yake ya Mkoa wa Dar es Salaam na maeneo jirani licha ya kuhamia rasmi jijini Dodoma toka Septemba 30,2022 wakati wa mahafali hayo yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI