Na Arnold Deogratias Matukio Daima Media Kagera
Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera imekamilisha zoezi la kuhamisha makaburi zaidi ya elfu tatu (3,000) kutoka katika eneo la Kishenge na kuhamisha katika Kata ya Buhembe, lengo likiwa ni kupisha mradi wa ujenzi wa jengo la ketega uchumi kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo yaani machinga.
Hayo yamebainishwa na Afisa mazingira wa Manispaa ya Bukoba ambaye ndio msimamizi wa zoezi hilo, Tambuko Joseph wakati akizungumza na vyombo vya habari ambapo ameeleza kuwa kulikuwa na makaburi 3,166 ambayo wameyaondoa yote na kuyahamishia katika eneo la Buhembe ili kupisha ujenzi wa Machinga Complex.
"zoezi la kuhamisha makaburi limekamilika kimsingi kulikuwa na makaburi 3,166 ambayo tumeyaondoa yote na tumeyahamishia eneo la Buhembe na kuzika masalia ya miili hiyo"
Aidha Bw.Tambuko ameongeza kuwa baada ya kumaliza zoezi la uhamishaji wa masalia ya miili iliyozikwa katika eneo hilo na kuifadhi katika eneo la Buhembe kinachofuata ni kujenga kaburi la pamoja na kujenga mnara inayoonyesha makaburi hayo.
"baada ya kumaliza kwa zoezi la kuhamisha makuburi kinachofuata ni ujenzi wa kaburi la pamoja kwa katika eneo la Buhembe ambapo majina ya maheremu yataandikwa katika mnara utakao jengwa"
Hata hivyo Afisa huyo ameeleza kuwa baada ya kumaliza suala la maziko ya masalia ya miili hiyo itafanyika misa ya kuwaombea maheremu hao ambayo itahusisha mathehebu mbalimbali na ndugu wa maheremu hao.
"baadae tutatangaza siku maalum kwa ajili ya kufanya misa ya kuwaombea maheremu hao itakayohusisha mathehebu mbalimbali"
Naomba baadhi ya wakazi wa manispaa akiwemo William Ruta na Japheth Cristian wamepongeza kwa zoezi hilo la kuhamisha makaburi kwani itasadia kukuza uchumi wa mji wa Bukoba na wafanyabiashara wadogo pale litakapojengwa jengo hilo.
Jengo la Machinga Complex linatarajiwa kuwawezesha wafanyabiashara wadogo yaani machinga kupata eneo la kufanya biashara zao na kuondokana na adha ya kupanga bidhaa zao pembezoni mwa barabara.










0 Comments