Header Ads Widget

MKUU WA USALAMA BARABARANI -NAMTUMBO AWATAKA WAFUNZI KUKATAA KUBEBWA NA MADEREVA BODABODA AMBAO HAWANA KOFIA ZA ABIRIA.

 

                                                Mgeni rasmi John Ntunde

                    Trafiki akiwafundisha wanafunzi namna ya kuvuka barabara

                                    Meneja uhusiano Mantra Khadija Pallangyo      

                                        Askari wa dawati la Jinsia Mwanaisha Moyo.

                            xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Na Amon Mtega,Namtumbo

MKUU wa usalama barabarani wa Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma John Ntunde amewataka wanafunzi wa Wilaya hiyo kukata kupanda Pikipiki (Bodaboda)wasiokuwa na kofia ngumu ya kwake na ya abiria.


 Ntunde  ambaye pia ni kaimu kamanda wa Wilaya hiyo ameutoa wito huo wakati akifungua mafunzo ya Elimu ya usalama barabarani kwa mwaka 2022 na 2023 ambayo  yamefanyika katika Shule ya Msingi ya Mtonya kata ya Likuyuseka Wilayani humo huku yakiwa yamefadhiliwa na kampuni ya Mantra Tanzania Rosatom inayojishughulisha na madini ya Uranium katika Wilaya hiyo.


 Kaimu kamanda huyo ambaye amekuwa mgeni rasmi kwenye mafunzo hayo yalioambatana na ukatili wa kijinsia amesema kuwa kumekuwepo na waendesha Bodaboda wasiokuwa na kofia ngumu za kuvaa abiria na kuwabeba abiria wakiwemo wanafunzi jambo ambalo limekuwa likihatarisha usalama kwa abiria hao pindi inapotokea ajali.


 Kufuatia hali hiyo kaimu kamanda huyo amewataka wanafunzi na Wananchi kuacha tabia ya kupanda Pikipiki hizo hadi pale waendeshaji watakapo badilika kwa kufuata sheria za usalama barabarani wa kujilinda yeye na abiria wake.

  

 Aidha katika hatua nyingine kaimu kamanda huyo akizungumzia suala la ukatili wa kijinsia amesema kuwa kumekuwepo na madereva Bodaboda kuwarubuni wanafunzi hasa wa kike kwa kujidai wanawapatia msaada wa usafiri (Lift)na kudanganyishia kapipi kwa malengo ya kutaka kuwaingilia kimwili (Kubaka) jambo ambalo amesema halitakiwi kufumbiwa macho.


 Kwa upande wake mkaguzi wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Namtumbo Kaunda Kaunda akisoma risala ameishukuru kampuni ya Mantra Tanzania Rosatom kwa kutoa ufadhili wa vifaa mbalimbali vya kufundishia kwenye somo la usalama barabarani jambo ambalo limefanya wanafunzi wengi kuwa na uelewa.


 Naye Meneja uhusiano wa kampuni ya Mantra Khadija Pallangyo amesema kuwa hadi sasa kwa miaka mitano mfululizo Wananchi na wanafunzi zaidi ya Elfu kumi na nne (14,000) wamefikiwa na Elimu hiyo na kuwa malengo kwa mwaka kwa mwaka huu ni kuzifikia shule 28 kwa kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika utoaji wa Elimu ya usalama barabarani kwa wanafunzi na Wananchi.


 Pia akitoa Elimu kwa Wananchi na wanafunzi kuhusu matumizi ya barabara kwa watembea kwa miguu katika Wilaya hiyo Nurdin Juma amesema kuwa watu wengi wanatembea kushoto mwa barabara jambo ambalo siyo sahihi hivyo wanatakiwa kutembea kulia kwa barabara ili kukabiliana na chombo cha moto kinachotokea mbele yao na kupata urahisi wa kukikwepa.


 Askari Nurdin pia ametoa Elimu ya namna ya kuvuka barabara sehemu zenye alama na ambazo hazina alama hasa barabara za Vijijini ambako ndiko kwenye changamoto ya kutokuwepo kwa alama kwenye maeneo mengi.


 Hata hivyo Askari Mwanaisha Moyo akitoa Elimu ya ukatili wa kijinsia amesema kuwa Wazazi wengi wamekuwa wakipoteza ushahidi wa watoto wao kubakwa kwa kumtuhumiwa kumalizana naye kienyeji jambo ambalo amesema halitakiwi na ikibainika hivyo Wazazi hao watachukuliwa hatua za kisheria.


 Mwanaisha ambaye pia anashughulika kwenye dawati la jinsia Wilayani hapo amesema kuwa ukatili umeota mizizi hadi sasa kunabaadhi ya wanaume wanapigwa na wake zao na wanaona aibu kuripoti kwenye dawati la jinsia hali inayowafanya washindwe kuwa na amani kwenye ndoa zao.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI