Header Ads Widget

WADAU WA UTALII WAKUTANA DAR, WAZIRI AFUNGUKA FURSA MPYA SEKTA YA UTALII

 


Na fatma Ally Matukio Daima APP Dar es y


Waziri wa Mali Asili na Utalii Balozi Dkt. Pindi Chana amesema kumekuwa na mwitikio mkubwa kwa watalii kutoka mataifa mbalimbali kwenda nchini Tanzania kutokana na filamu ya Royal Tour hivyo nifursa kwa wafanyabishara wa Sekta ya utalii kukuza biashara zao kupitia Sekta hiyo.


Kauli hiyo ameitoa jijini Dar es Salaam alipokua katika mkutano wa wataalamu wa mafunzo ya utalii kutoka vyuo vya utalii ambapo amesema 

kwa sasa sekta ya utalii ni soko kubwa la kuzalisha ajira na kuongeza pato la taifa hivyo jitihada mbalimbali zinaendelea kufanyika kuboresha Sekta hiyo.


Amesema kuwa, Serikali kwa kushirikiana na wadau wa utalii wameendelea kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo nchi hususani kusini mwa Tanzania ili kuwavutia wawekezaji, huku akiwataka waeekazaji wa hoteli kuwekeza katika hifadhi za taifa zilizopo katika mikoa ya kusini nwa Tanzania katika Masuala ya hoteli nasehemu za kulala wageni ili kuweza kuboresha Sekta hiyo.


”Maeneo ya Uwekezaji wa Hoteli na sehemu za kulala wageni bado ni hitaji kubwa katika utalii wa kusini mwa Tanzania hivyo wawekezaji wachangamkie fursa hii kwani wataweza kuongeza ajira kwa wingi na kukuza uchumi wa nchi ” amesema Balozi Chana.


Kwa upande wake Kaimu Afisa Mkuu wa Chuo cha Utalii Dkt. Florian Mtei amesema katika mkutano huo watapitia tafiti zilizofanywa na wataalamu kutokana nchi mbalimbali ikiwemo Afrika Kusini ili kukabiliana na changamoto zizosababisha janga la Covid 19.



"Kipindi ulipoingia ugonjwa w covid 19 mataifak mengi yaliathirika nasekta nyingi zilitetereka ikiwemo sekta hii ya utalii, watalii walipungua sana hivyo pamoja na mambo mengine Mkutano huu pia utaangalia hangamoto zilizosababishwa na janga la Covid 19 na jinsi ya kukabiliana nazo ili kukuza sekta ya utalii"amesema


Aidha, amesema kuwa kupitia mkutano huo wataweza kuweka mikakati kama nchi kuangalia njia gani wanazoweza kufanya kuepukana na majanga kama Covid 19 yanayoisumbua duniani Ili kukuza Sekta ya utalii.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI