Header Ads Widget

WALIMU ZINGATIENI MIIKO NA MAADILI YA KAZI YENU"_MKWAMA

 


NA HAMIDA RAMADHAN DODOMA MATUKIO DAIMA APP DODOMA


WALIMU Nchini wametakiwa kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia miiko na maadili ya kazi ili kuongeza tija katika ufundishaji na hivyo kuleta ubora wa elimu hapa nchini.


Katibu Mkuu Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) Mwalimu Palina Mkwama ameyasema hayo leo Jijini hapa wakati akizungumza na waandishi kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Tume hiyo.


Amesema,chombo hicho kimekuwa kikitoa elimu kwa walimu ili wafanye kazi yao kwa kuzingatia maadili huku akisema pampja na jitihada hizo lakini bado kuna walimu ambao wamekuwa hawazingatii miiko na maadili ya kazi yao.


Kwa mujibu wa Katibu Mkuu huyo,walimu hao wasiozingatia maadili ya kazi yao ,huilazimu TSC kuwafikisha kwenye mamlaka zao za nidhamu kwa mujibu wa kanuni kwa ajili ya kushughulikiwa kwa kuchukuliwa hatua za kinidhamu ili kuwanusuru watoto na kuwafanya wapate huduma iliyokusudiwa.


Amesema Tume hiyi imejikita katika zaidi katika elimu kwa walimu ili watekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria ,kanuni na taratibu ambapo watendaji wa wilaya wamekuwa wakifika shuleni kutoa elimu kwa walimu kuhusu ajira na maendeleo ya walimu pamoja na maadili na kujiepusha na makosa ya kinidhamu kwa walimu


Aidha ametumia nafasi hiyo kuwashukuru na kuwapongeza walimu kwa kazi kuwa wanayoifanya ya kutoa elimu kwa watoto hapa nchini huku akiwasihi kwamba TSC ipo pamoja nao kuhakikisha walimu wanapata stahiki zao .


“Hapa nasisitiza kuwa TSC ni chombo chenu kimeundwa kuwahudumia ,hakipo kwa ajili ya kuwafukuza kazi walimu la hasha ,bali kimeundwa kwa ajili ya kuongeza ufanisi wa kuwahudumia walimu katika ajira zao ,maadli ya utumishi wao kwa kuhakikisha kwamba walimu wanafanya kazi zao kwa kuzingatia miiko ya maadili ya kazi ya ualimu na maendeleo yao katika utumishi wa umma,"amesema Mwalimu Mkwama.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI