Header Ads Widget

VIONGOZI WATAKIWA KUZINGATIA MISINGI ILIYOACHWA NA NYERERE.



 VIONGOZI nchini wametakiwa kuzingatia misingi ya uongozi kama alivyokuwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere kwa kuwa na maono ya kuwaletea maendeleo wananchi.

Hayo yamesemwa na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Abdulrhman Kinana kwenye shule ya uongozi ya Mwalimu Nyerere Kwa Mfipa Mjini Kibaha wakati akifungua mdahalo wa kumbukizi ya miaka 23 ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mdahalo ulioandaliwa na Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kwa kushirikiana na shule hiyo.

Kinana amesema kiongozi bora ni yule anayeongoza kwa maono na si kuongoza kutokana na matukio na kiongozi bora siyo anayeendana na hali ya hewa, kufurahisha watu na kusukumwa.

Kwa upande wake Makamu mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Petro Kimiti amesema kuwa wanatarajia kujenga makao makuu ya taasisi hiyo ambapo kutakuwa na historia yake na yale aliyoyafanya na misingi aliyoyasimamia.

Naye Mkuu wa Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere Profesa Joyce Chijoriga amesema kuwa wana Mpango wa kutoa mafunzo kwa Makatibu tawala, wakuu wa Wilaya, wakurugenzi wa Halmashauri ili nao wapate mafunzo ya uongozi.

Abbas Mwalimu ambaye ni Mwalimu wa chuo cha Diplomasia alisema kuwa kuwe na sheria au mfumo wa kupata viongozi kupimwa kabla ya kuwa kiongozi akisiwe kwa kupita kwenye chuo hicho mifumo ya kuongeza uwazi uwajibikaji na utawala wa sheria na kupambana na rushwa pia ardhi itumiwe kwa maendeleo ya wananchi.

Naye Fatma Said Ally aliyewahi kuwa Waziri amesema kuwa Rais Samia Suluhu ameonyesha kuwa uongozi kwa mwanamke inawezekana na ilionekana kama zamani ilikuwa ni mfumo dume lakini Nyerere aliona tangu miaka hiyo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS