Header Ads Widget

MAKABIDHIANO YAFANYIKA: ACC AWEDA MKUU MPYA HIFADHI YA TAIFA MILIMA MAHALE


Na. Jacob Kasiri - Mahale.

Kubadilishana vijiti katika uongozi ni suala la kawaida linalolenga kuleta ufanisi ndani ya taasisi za umma na kuendeleza yale mazuri yaliyoasisiwa na mtangulizi anayekabidhi madaraka kwa kiongozi mpya.

Hayo yamefanyika  Januari 15, 2026 katika Hifadhi ya Taifa Milima Mahale ambapo Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi Simon Awada alipokabidhiwa ofisi na kuwa Mkuu Mpya wa Hifadhi hiyo iliyopo Magharibi mwa Tanzania ikisifika kwa  kuwa na idadi kubwa ya wanyamapori aina ya Sokwemtu kuliko eneo lolote lililohifadhiwa nchini Tanzania.

Wakati wa makabidhiano hayo, Mkuu wa Hifadhi anayeondoka Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi Halid Mngofi aliwashukuru maafisa na askari kwa ushirikiano wao katika kuimarisha uhifadhi wa wanyamapori adimu na maliasili nyingine zinazojumisha za majini na zile za nyika zinazopambwa kwa safu za milima na mabonde. 

Adhia, pia Kamishna Mngofi aliwataka na kuwasihi makamanda hao kumpa ushirikiano Mkuu mpya wa hifadhi ili kufikia malengo ya TANAPA na Taifa kwa ujumla. 

Kamishna Aweda awali kabla ya kuja Hifadhi ya Taifa Milima Mahale alikuwa Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Burigi-Chato na Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi Halid Mngofi anahamia Hifadhi ya Taifa Burigi-Chato kuwa Mkuu mpya wa Hifadhi hiyo.






Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI