Header Ads Widget

MKUU WA MKOA WA MTWARA ASHUHUDIA MIKATABA 18 YA UJENZI WA BARABARA.

 


Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abass Ahmed amezitaka kampuni 18 zilizosaini mikataba na Wakala wa barabara za vijijini na mijini (TARURA) Mkoa wa Mtwara kuhakikisha miradi yote 18 yenye thamani ya Shilingi bilioni 8.2 inakamilika kwa wakati. 


Kauli hiyo ameitoa leo katika hafla ya uwekaji wa saini na kuwataka kufanyakazi kwa uadilifu ili kuepuka dosari zinazoweza kuchelewesha kukamilika kwa miradi hiyo.


"Nawapongeza wakandarasi wazawa fanyeni kazi kizalendo na kwa uaminifu mkubwa shirikisheni wananchi katika maeneo mnayofanyia kazi hii Itasaidia kuboresha utendaji kazi wenu na kuwa na ulinzi thabiti kwenye miundombinu tunayoifanyia kazi" alisema  Kanal Abbas


Nae Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Mtwara Enock Ngairo alisema kuwa usimamizi bora wa miradi inaokoa fedha za Serikali na kuwa na miundombinu Bora yenye viwango. 


Wakandarasi wanapaswa kusimamia miradi wenyewe sio kuwaachia watu wasio watalaamu wao hawakai na hawatilii mkazo kazi hizi  ili uwe Bora na upate kazi nyingi hauna budi kusimamia kazi yako kwa ufanisi mkubwa ili kuepuka mazingira ya rushwa lazima tuwe wazalendo" alisema Ngairo


Kwa upande wake Meneja wa Wakala wa Barabara mijini na vijijini Tarura Mkoa wa Mtwara  Mhandisi Zuena Mvungi alisema kuwa Wakandarasi wote wamekidhi vigezo vinavyotakiwa.


"Wapo walioleta maombi lakini hayakuwa na vigezo ambapo tulipokea maombi 330 lakini hayakuwa n sifa wengi wao walioleta maombi wakati nyaraka zikiwa pungufu wengine walioleta zikiwa hazisomeki na wengine zenye mashaka na kuwafanya wakose sifa za kupata zabuni hiyi"  Eng Mvungi


Nae Meneja mahusiano wa mikopo mikubwa ya Benki ya NMB Credo Malongo Alisema kuwa ili kuwezesha Wakandarasi kupata mikopo kwa wakati wamejengea uwezo matawi yote Kanda ya Kusini. 


"Tunafanyakazi na Wakandarasi kwakuwapa mikopo ili kundana na Kasi ya utendaji kazi wa Wakandarasi tumejengea uwezo matawi yetu ambapo mkandarasi anaweza kupata mkopo mpaka shilingi milioni 200 katika tawi" Alisema  Malongo





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS