Header Ads Widget

VIONGOZI WA DINI MBEYA WAJENGEWA UELEWA BIMA YA AFYA KWA WOTE

 



Na Matukio daima media, Mbeya


VIONGOZI wa dini mkoani Mbeya wameipongeza serikali kwa kuja na mpango mahususi wa kusaidia jamii kwa kuleta muswada pendekezwa wa  wa sheria ya Bima ya afya kwa wote kwani  sio watanzania wote wana uwezo wa kiuchumi wa kuwawezesha  kupata matibabu .


Kauli hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti wa kamati tendaji ya CCT mkoa wa Mbeya Padri. Daudi Sichinga wakati wa mafunzo  ya kujengewa  uelewa kuhusu muswada pendekezwa  wa Sheria ya Bima ya Afya kwa wote yaliyofanyika katika ukumbi wa  Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya.


Padri Sichinga amesema kuwa serikali ya awamu ya sita  chgini ya Rais Samia Suluhu Hassan imefanya jambo la msingi sana hasa ukizingatiwa sio watanzania wote ambao wana uchumi ambao utawawezesha kupata matibabu .



“Mswada huu pendekezwa  wa sheria ya Bima ya afya kwa wote itasaidia wananchi wengi kuwa na uhakika wa matibabu kabla ya  kuugua hivyo bima hii ya afya kwa wote imekuja muda mwafaka  tunaamini sisi  viongozi wa dini tunaenda sasa kuelimisha waumini wetu ili waone umuhimu wa jambo hili kwao  na tunaamini wengi wao watalipokea”amesema.


Kwa upande wake  Sheikh Ibrahim   Bombo, alipongeza  Wizara ya afya kupitia uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya kwa kuona umuhimu wa kuwajengea uelewa viongozi wa Dini na kusema  katika Dini swala la Amani, Chakula na Afya ni muhimu kwa kuwa waumini ili waweze kupata maagizo ya Mwenyezi Mungu ni lazima wawe na afya njema.


Shekhe Bombo amesema  suala la afya ni muhimu kwa kila mwananchi hivyo kama viongozi wa wadini watakikisha kila muumini elimu hiyo inamfikia kikamilifu .


Aidha, Mchungaji kutoka Jumuiya ya Makanisa kipentekoste Tanzania, Bi. Erika Mwakyolile amesema swala la Sheria ya Bima ya Afya kwa wote ni kama Serikali ilichelewa sana, wao kama  watumishi wa Mungu watashirikiana na Serikali bega kwa bega kuelimisha jamii kwa kuwa afya ni muhimu hivyo jamii kama vile inavyochangia sherehe nyingine, pia wachangie   bima ya   afya kwa kuwa  ni muhimu kuliko sherehe kwa ustawi wa afya zao.




“Na nitoe rai kwa watu wote, hata kwa Serikali kwamba ni kweli tulichelewa sana na tunashukuru kwa muamko huu, sisi kama watumishi wa Mungu wa Dini mbalimbali ya Kiislam na Kikristo tunaamka kwa nguvu zote kwenda kuelimisha watu wetu” Mchungaji Erika Mwakyolile


Akizungumza katika mafunzo hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya Dkt. Godlove Mbwanji amewashukuru viongozi wa Dini wa mkoa wa Mbeya kwa umoja na ushirikiano waliouonyesha katika kuendelea kuitakia heri Hospitali.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI