Header Ads Widget

MTAKUWWA MAGU YAKUMBUSHWA KUELIMISHA JAMII DHIDI YA UKATILI WA KIJINSIA


Rai imetolewa kwa Kamati ya Kupinga Ukatili wa Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) Wilayani Magu kuweka mkazo  elimu kwa Jamii kuhusu namna ya kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia ambavyo vimeshamiri wiilayani humo.

Rai hiyo imetolewa leo Julai 1, 2026 na Mwenyekiti mwenza wa Kamati ya MTAKUWWA ngazi ya mkoa wa Mwanza Bw. Yassin Ally wakati wa kikao cha pamoja na Kamati ya wilaya hiyo kilicjofanyika kwenye ukumbi wa mikutsno wa Halmashauri ya Magu,amesema vitendo vya ukatili vimekuwa tishoo katika maendeleo ya wananchi

Ametolea mfano katika sekta ya elimu bado kunahitsjika jitihafa za ziada kutokana na baadhi ya walimu kuzikimbia shule wanazofindisha kutokana na kuingiliwa kimwili kishirikina hali ambayo imesababisha taharuki.

"Hali ni mbaya tushikamane kutokomeza hali hii tusikae maofisini twendeni tukawape elimu jamii,vinginevyo tutazidi kurudi nyumba kimarndeleo" amesisiriza Mwenyekiti mwenza.

Ameongeza kuwa baadhi ya wazazi wanatoa mafundisho potofu kwa watoto zao wa kike kuchora madudu kwenye mitihani yao ya kumaliza ili wajifelishe kwa makusudi na waishie kuolewa.

Afisa Ustawi wa Jamii mkoani Mwanza Baraka Makona amesema Kamati hiyo ya MTAKUWWA Mkoa wa Mwanza inafanya ziara kwenye wilaya zote mkoani humo ili kuona mipango ya utekelezaji na changamoto wanazokabiliana nazo.

Awali akitoa taarifa fupi ya utekelezaji wa MTAKUWWA Wiilayani Magu AFISA Ustawi wa Jamii wiilayani humo Bi.Coletha Sanga amesema katika kupambana na umasikini ndani ya jamii wametoa mikopo kwa vikundi 13 wenye gharama ya zaidi ya shs.milioni 143.

Kamati ya MTAKUWWA ngazi ya mkoa itaendelea na ziara yake Alhamisi hii kwa kutembelea Halmashauri ya Ilemela.

 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI