NA CHAUSIKU SAID, MATUKIO DAIMAAPP MWANZA.
Vijana wanaohitimu elimu ya Msingi na Sekondari wameshauriwa kutojihusisha na makundi ya aina yeyote ya kiarifu yatakayosababisha washindwe kuendelea na masomo yao.
Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Jumanne Sagini alipohudhulia mahafali ya tatu kwa darasa la Saba na ya tisa Kwa darasa la pili la awali katika shule Blessing model medium na kueleza kuwa wahitimu hao wanapaswa kuishi katika misingi ya malezi waliyopatiwa na walimu wao na kuendeleza kwenye jamii.
Sagini amewaasa wazazi na walezi kutowaacha vijana waliohitimu kujiunga na makundi Hayo yasiyofaa kwa sababu atakapokamatwa Sheria itafuata mkondo wake na haitaangalia umri atakaokuwa nao mtuhumiwa na atahukumiwa kulingana na makosa yake.
" Lakini hatutegemei kuona vijana wetu waliomaliza shule wanajiingiza kwenye vitendo viovu vinavyoweza kuhatarisha maisha yao" Alisema Sagini.
Amesema kuwa wamegundua Kuna baadhi ya watoto wana tabia zisizofaa kwenye jamii na kusababisha uharifu, mauaji hivyo kupelekea kuitwa majina yasiyofaa Kama panya road ili kujitenga na mambo Kama hayo badala yake waende kwenye mafunzo wapate ujuzi utakaowasadia kwenye maisha.
" Nafahamu kuwa maeneo mengi watoto wameishahitimu, na waliomaliza darasa la Saba wengi ni wadogo wadogo hakuna watakaojiingiza kwenye makundi ya ajabu" Alisema Sagini.
Aidha Kwa upande mwingine amesema kuwa wanategemea kuona Nchi inaendelea kuwa na amani na usalama wa watu na Mali zao .
" Watanzania wanapaswa kuendelea kuwa watulivu Kwa kutofanya mambo yanayovunja Sheria,na sisi tunasema anayefanya uharifu nakuvunja Sheria atakuwa mteja wa jeshi la polisi,mahakama na Gereza Kwa ujumla" Alisema Sagini.
Ezekiel Mollel ni mkurugenzi wa Blessing model school ameeleza kuwa watahakikisha wanaendelea kutoa elimu bora Kwa kufuata ilani ya chama Cha mapinduzi Kwa kutoa hamasa Kwa walimu ili waweze kufundisha Kwa ufasaha na wanafunzi kuwa na ufaulu utakaoridhisha.
Mollel ameeleza kuwa kutokana na Hayati Baba wa Taifa alipiga vita maadui watatu ujinga, maradhi pamoja na umasikini hivyo wanabudi kuunga juhudi hizo Kwa kuwafundisha watoto Kwa nguvu zote ili waweze kuwa na ufaulu utakaowasadia katika maisha yao.
" Sisi Kama shule ya Blessing binafsi tunaunga mkono kauli ya baba wa Taifa na ilani ya chama Cha mapinduzi" Alisema Mollel.
Mkurugenzi wa Blessing model school Ezekiel Mollel


.jpeg)








0 Comments