Header Ads Widget

UZALISHAJI WA SUKARI KUONGEZEKA NCHINI

 



Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma



MKURUGENZI Mkuu Bodi ya Sukari Tanzania Profesa Kenneth Bengesi amesema, katika kipindi cha Miaka miwili ijayo nchi ya Tanzania haitakuwa na uhaba wa sukari kwani uzalishaji utaongezeka kutoka Tani 380,000 za Sasa hadi kufikia Tani 756,000 ifikipo Mwaka 2025/2026.


katika kipindi hicho Mwaka 2025/2026 uhaba wasukari utaisha kutokana na Mikakati mbalimbali iliyowekwa na bodi hiyo ya kuongeza viwanda vya ndani.


Mkurugenzi Mkuu huyo aliyasema hayo  Jijini Dodoma wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa Majukumu ya Bodi hiyo na mwelekeo wa utekelezaji kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023.


Prof.Bengesi amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia suluhu hassan imedhamiria kuongeza uzalishaji wa sukari nchini kwa kujenga viwanda vingi ili kuongeza ajira kwa Watanzania.


Mkurugenzi huyo amebainisha kuwa kwa sasa Serikali inatumia fedha nyingi kuagiza sukari kutoka nje ya nchi ambapo serikali inatumia zaidi ya dolla million 150 ambazo ni zaidi ya billion 300.


Amesema serikali inatumia zaidi ya dolla million 150 ambazo ni zaidi ya billion 300 kuagiza sukari nje ya nchi jambo ambalo linawezekana kuzuilika endapo tutadhamiria kwa pamoja kuongeza uzalishaji wa sukari nchini kwa kujenga viwanda vingi jambo ambalo pia litaongeza ajira kwa Watanzania. 


 "Sisi kama chombo cha udhibiti chenye ufanisi na kinachoweza kuhudumia na kusaidia tasnia ya sukari kufikia ushindani na uendelevu unaotakiwa tuna jukumu la kuisaidia serikali kupunguza gharama za uagizaji wa Sukari kutoka nje na ili tufanikiwe ni lazima tuwekeze kwenye ujenzi wa viwanda,"Prof.Bengesi


Bodi ya Sukari Tanzania kwa kuongozwa na kanuni za kutoa huduma kwa usawa, huduma bora na uadilifu, inalenga kuunda, kudumisha na kudhibiti mazingira ambayo yanawafaa wawekezaji wa sukari kuzalisha miwa, sukari na bidhaa zinazohusiana kwa ufanisi na kwa faida.


Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI