Header Ads Widget

MILIONI 60 ZAANZA UJENZI WA MADARASA SEKONDARI YA MATIPWILI.

 




HALMASHAURI ya Chalinze Wilayani Bagamoyo imetoa kiasi cha shilingi milioni 60 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa matatu kwenye shule ya sekondari ya Matipwili iliyopo Kata ya Mkange.


Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Benjamin Nyamatwema aliyasema hayo kwenye mahafali ya 13 ya shule hiyo.


Nyamatwema alisema kuwa ujenzi huo umeshaanza kuchimbwa msingi ambapo madarasa hayo matatu yatagharimu kiasi cha shilingi milioni 60.


"Madarasa hayo yatajengwa na yatapokea wanafunzi watakaoanza kidato cha kwanza mwakani fedha ambazo zimetolewa na serikali,"alisema Nyamatwema.



Alisema kwa niaba ya watumishi wenzake wanamshukuru Rais Samia Suluhu kwa kazi kubwa ya kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu bora kwa kuwa na miundombinu mizuri.


Naye Diwani wa Kata ya Mkange Mohamed Gelegeza alisema kuwa Wilaya inaendelea na mikakati inayolenga kuboresha elimu ikiwemo kuwadhibiti wanafunzi wanaozurura mitaani nyakati za jioni.


Gelegeza alisema kuwa kwenye Kongamano la elimu lililofanyika hivi karibuni  Mkuu wa wilaya Zainab Abdallah ameagiza mambo kadhaa ikiwemo wanafunzi kula shuleni, pia kutoonekana mitaani kuanzia saa moja usiku na kutoshiriki kwenye vigodoro.


Naye Mgeni rasmi kwenye mahafali hayo Bori Amiri mwakilishi wa kampuni ya Kisampa Camp inayojihusisha na utunzaji wa mazingira alisema kuwa uongozi wanataraji kufanya jambo shuleni hapo ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Serikali.



Akisoma taarifa ya wahitimu Maria Tesha ilionyesha kuongezeka k kwa ufaulu, utunzaji mazingira licha ya kuwa na changamoto za upungufu wa vitabu, bwalo la chakula na mfumo wa umeme wa jua.


Tesha alisema kuwa shuleni hapo wana umeme wa jua ambao kutokana na kutumika muda mrefu umechakaa hivyo  taa kuzima mapema hali inayosababisha washindwe kuutumia vizuri kujisomea jumla wahitimu 73 waliagwa shuleni.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI