Na Gift Mongi, Moshi
Wadau wa maendeleo na watu binafsi wamehimizwa kuendelea kushirikiana na serikali kwa kuchangia vifaa vya misaada ya kibinadamu wakati wa maafa ili kupunguza madhara ambayo yanaweza kujitokeza ikiwemo vifo na ulemavu
Hali kadhalika serikali imewndelea kutambua michango hiyo ambayo kwa namna moja ama nyingine imetajwa kuwa ni msaada kwa jamii na kuwa ni vyema kuendelea kujitokeza badala ya kuiachia serikali pekee
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Ummy Nderiananga ametoa kauli hiyo mjini hapa mara baada ya kukagua ghala la kuhifadhi vifaa vya misaada ya kibinadamu kwa Kanda ya kaskazini lililopo eneo la Chekereni wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro
Amesema uungwaji mkono wa serikali kutoka kwa wadau unasadia wananchi kufikiwa na huduma kwa haraka kutokana na majanga yaliyojitokeza ambayo husabababisha madhara kama vifo, ulemavu wa kudumu, mali kuharibika pamoja na miundombinu.
“Nitoe wito kwa wadau na watu mbalimbali ambao wanaguswa kushirikiana na serikali kwa kutoa vifaa wafanye hivyo pengine ngazi ya Wilaya, Mkoa na hata kijiji ili tuwe navyo vya kutosha ili yanapotokea tunatoa msaada kwa haraka,” amehimiza Ummy.
Pia amesisitiza utunzwaji wa magahala hayo hatua itakayosaidia vifaa hivyo kudumu kwa muda mrefu na kuwa tayari kutumika pindi vinapohitajika katika maeneo yenye maafa.
"Naomba vitunzwe ili viweze kuwa na maana pindi vitakavyohitajika maa a visipotunzwa ni sawa na Kama hakuna vifaaa hivyo"amesisitiza Ummy
Aidha ameupongeza uongozi wa mkoa wa Kilimanjaro kwa utayari wa kutoa msaada wa kibinadamu kwa wananchi wanaokumbwa na maafa kwa lengo la kuwasaidia kurejea katika hali yao ya awali.
Kwa upande wake mwakilishi wa katibu tawala msaidizi uchumi na uzalishaji mkoa wa Kilimanjaro ambaye ni Afisa mifugo katika mkoa huo James Shao amesema ghala la kanda ya kasikazini linahudumia Mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Tanga.
0 Comments