Header Ads Widget

AJERUHIWA VIBAYA BAADA YA KUKATA NGUZO YA UMEME KWA SHOKA .

Na Lucas Raphael,Tabora

Kijana mmoja aliyetambulika kwa jina la Kigodi Juma (24)amejeruhiwa vibaya maeneo ya mwili wake baada ya kupingwa na shoti ya umeme alipokuwa akifanya hujuma ya kukata  nguzo ya umeme kwa kutumia shoka.  

 

Mtu  huyo ambaye ni mkazi wa kijiji cha Nkiniziwa kilichopo  Wilaya ya  Nzega  Mkoani Tabora .

 

Akitoa ufafanuzi  wa tukio hilo  Afisa mtendaji wa kata ya  Nkiniziwa  Hamisi  Bundu alisema kijana huyo alitenda tukio hilo usiku wa kuamkia Oktoba 11,2022 ambapo  kunako majira  hayo  ya usiku walishitushwa na kukatika kwa huduma ya umeme.

 

Alisema kijana huyo kabla ya kuanza kukata  nguzo hiyo alirusha waya uliokuwa umefungwa vipande vya miti kwa ajili ya kupigisha shoti  ili umeme uweze kukatika ili apate urahisi wa  kuangusha nguzo hiyo  bila wasiwasi wa kujeruhiwa na umeme  pasipo kujua kama umeme bado ulikuwa haujakatika .

 

Hamisi  Bundu aliendela kusema kwamba  baada ya kijana huyo kukata nguzo hiyo na kisha kupigwa shoti na moto kali wa umeme kutokea kwenye la eneo la tukio hilo.

 

Alisema kwamba  kijana huyo ambaye alishambuliwa vibaya  na shoti ya umeme alikimbizwa katika kituo cha afya  Busondo ambacho kipo jirani na kijiji hicho ambapo kwa sasa anaendelea na matibabu.

 

Naye  kaimu Mganga wa kituo cha afya Busondo Juma Sosoma alikiri kumpokea majeruhi huyo ambaye aliangusha  nguzo ya umeme.

 

Alisema kwamba   licha ahuweni aliyonayo kwa sasa  ataandikiwa rufaa ya kwenda  katika  hospitali kubwa kwa ajili ya vipimo  zaidi  vya  ndani ya mwili kutokana na kuumia vibaya  katika maeneo ya miguu,shingo ,usoni  na kwenye mikono.

 

Wanachi wa kijiji  cha Nkiniziwa  walisema  mpaka sasa bado  wanaendelea kuathirika na ukosefu wa huduma ya umeme huku tukio hilo la kukatwa kwa nguzo likitajwa kuwa ni la pili katika eneo hilo hilo.

 

Kaimu meneja   wa shirika la umeme nchini TANESCO  katika Mkoa wa Tabora  Mhandisi  Hamisi Maganga  alisema shirika linaendelea  na ufatiliaji wa kina  juu tukio hilo  huku  akiwaonya  vikali wananchi dhidi  vitendo vya kufanya kuhujumu miundombinu ya umeme .

 

Kamanda wa Polisi Richard Abwao alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema kwamba mtuhumiwa anaendelea na matibabu licha ya kuumia vibaya sehemu mbalimbali za mwili wake .

 

Alisema kwamba jeshi la polisi linaendelea na upelelezi wa kuwatafuta watuhumiwa wengine walioshiriki katika kuharibu miundombinu ya umeme na kuongeza hii ni mara ya pili kwa nguzo ya umeme kukatwa kwenye eneo hilo



NI miundombinu ya umeme  iliyoaribiwa kwa kutumia shoka na kusababisha wananchi wa wilaya ya nzega na maeneo jirani kukosa huduma ya umeme wanaoneka ni wataalam wa shirika la umeme Tanesco mkoani Tabora

 
Kijana Kigodi Juma (24)ambaye amewalazwa katika kituo cha afya Busondo akitibu majeraha baada ya amejeruhiwa vibaya maeneo ya mwili wake

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI