Header Ads Widget

SERIKALI YASAMBAZA MICHE AINA MPYA YA MAJANI YA MALISHO YA MIFUGO

 


SERIKALI  imesambaza Miche ya aina mpya majani ya malisho kwa mifugo aina ya Juncao ni jani kutoka nchini China katika mikoa nane nchini ikiwa ni mkakati wa kusaidia Wafugaji kupata malisho Bora hasa kipindi cha ukame na kiangazi.


Hayo yamesemwa na Meneja wa Shamba la Malisho ya mifugo la Vikuge Kongowe Kibaha mkoani Pwani Reuben Ngailo alisema jani hilo lenye majani mengi nyasi za malisho mengine tuliyonayo nchini.


Alisema majani ya juncao ambayo yametengenezwa kutokana na jani la Tanzania aina ya mabingobingo au elephant glass na kuchanganywa na  aina ya jani la huko China ambalo limeletwa nchini na serikali lizalishwe ilikusaidia chakula cha mifugo nchini.



Ngailo alisema jani hilo lililetwa shambani hapo kwa majaribio lakini kwa Sasa tayari majaribio yamekamilika kwani majani hayo yamekubaliana na hali ya hewa ya nchi yetu.


Alisema tayari wameanza maandalizi ya kuongeza eneo la hela nne ilikuhakikisha mbegu hiyo inazalishwa kwa wingi tayari kwa uendeleza usambazaji.


Aidha Meneja huyo wa Shamba la malisho ya mifugo la Vikuge aliwataka Wafugaji kujitokeza kwa wingi kuchukua mbegu hizo wakapande mashambani kwao ili waweze kunusuru mifugo yao hasa kipindi cha ukame na kiangazi.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI