Header Ads Widget

VIJANA NA WANAWAKE WAKULIMA WAPIGA MSASA MABADILIKO TABIA NCHI



Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma

KUTOKANA na tatizo la mabadiliko ya tabia nchi ambayo imeendelea kuathili nchi kila siku na hata duniani kwa ujumla Vijana na wanawake wakulima kutoka Mikoa yote ya Tanzania wamekutana Jijini Dodoma lengo ikiwa ni kuona namna ya kukabilina na tatizo hilo. 


Vijana na Wanawake hao wakulima ni wawakikishi kutoka kwenye makundi ya vijana na wanawake ambao wametoka  maeneo mbalimbali ambapo kwa Upande wa Wanawake wametoka katika  jukwaa la Wanawake Tanazania.


Akiongea na waandishi wa habari Mratibu wa vijana kutoka Shirika la Actionaid Tanzania Arif Fezal amesema lengo la mkutano huo ni pamoja na kuwakutanisha Wanawake hao wakulima na vijana ambao wametoka katika mikoa tofauti tofauti Kujifunza dhana ya mabadiliko ya tabia nchi kwa hapa nchini Tanzania na namna gani kama Wanawake wakulima  na vijana wanawezaje kujianda na mabadiliko hayo.


Alisema Kama tunavyofahamu hivi karibuni kutafanyika Majadiliano ya kidunia ya mabadiliko ya tabia nchi yani COP27 Mkutano utakao fanyika nchini Egypt ambapo Marais wa dunia na wanaharakati na wadau mbalimbali wa Masuala ya tabia nchi na Mazingira wanakutana kujadili na kupanga Mipango ya kukabilina na kuhilimili hali hiyo.


"Hivyo tumewakutanisha vijana na Wanawake hawa wakulima lengo nin kuzungumza na kujifunza na kuangalia kwa uzoefu wao na kuandaa mawazo yatakayozungumzia Hali ilipo kwao na wanatarajia nini baada ya huo mkutano wa COP 27," Alisema .


Kwanini kundi la Wanawake na vijana ni kwasababu athali ya tabia nchi inapotokea kundi kubwa linaloathika ni Wanawake na vijana watoto na Watu wenywe Ulemavu.


Kikubwa tumewafundisha ili kukabiliana na mabadiliko hayo kwa kujikita kwenye kilimo asilia na kilimo Cha umwagiliaji Alisema Fezal


Naye Seleamani majangwa katibu Mkuu Activista alisema vijana wamekuwa wakiathilika na mabadiliko ya tabia nchi na eneo kubwa ambalo limekuwawakihangaika nalo kutokana na mabadiliko ya tabia nchi ni kilimo .


"Kwanini ajira ni kutokana na kwamba vijana wengi wamekuwa wakijikita katika kilimo lakini kilimo hicho Kumekuwa kikiwatupa mkono kutokana na mabadiliko hayo, " Alisema


Naye Cecilia Remmy mkulima  kutoka mkoa wa Morogoro Kilosa ameitaka Serikali iweke Bima ya mazao ili inapotokea majanaga Kama mafuriko na kupelekea mazao kuharibika waweze kulipwa lakini pia Serikali iwasaidie miundombinu ili wananchi waendelee kuwekeza kwenye kilimo .


Naye Said Eddes Mkoba kutoka Kilwa Alisema Mkutano huo unakwenda kuwaweka vijana katika Hali ya kuweza kukabilina na kuhilimili mabadiliko ya tabia nchi.


" Sisi Kama vijana Tunashukuru Kuwa wamoja na kujadili Masuala mazima ya mabadiliko ya tabia nchi ambapo baada ya Kikao hichi tutaweza Kutoa maoni yetu ambayo tunauhakika mawazo yetu yatapelekwa huko katika Mkutano Mkubwa COP 27  Nchini Egypt," Alisema.


Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI