Header Ads Widget

NMB YAKABIDHI MISAADA YA VIFAA MBALI MBALI

 


Na Fadhili Abdallah,Matukio DaimaAPP Kigoma

Benki ya NMB imekabidhi misaada ya vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 20 kwa ajili ya matumizi ya wanafunzi wenye mahitaji kwenye shule ya msingi ya wanafunzi wenye mahitaji maalum (Walemavu) ya Bitale iliyopo Halmashauri ya wilaya Kigoma  mkoani Kigoma

 

Vifaa hivyo vimekabidhiwa kwa Mkuu wa mkoa Kigoma, Thobias Andengenye kwa niaba ya shule hiyo na Mkuu wa idara  ya biashara na huduma za serikali kutoka Bank ya NMB, Vicky Bishubo



Bishubo alivijataja misaada iliyotolewa kwa wanafunzi wa shule hiyo kuwa ni pamoja na vitanda vya chuma15, Magodoro 30,Madawati 100 na Mabati 185 vifaa vyote vikiwa na thamani ya  ya shilingi milion 20.

 

 Bishubo alisema kuwa kutolewa kwa misaada hiyo ni sehemu ya mpango wa benki hiyo  kuunga mkono jitihada za serikali katika kupeleka huduma kwa wananchi na kwamba hiyo imetekelezwa kupitia mpango wa benki hiyo unaojulikana kama kurudisha faida kwa jamii.


Meneja huyo wa NMB alisema kuwa benki hiyo imetoa msaada huo baada ya kupokea maombi kutoka kwa viongozi wa serikali ya wilaya Kigoma kupitia shule hiyo na hivyo kuweza kupeleka misaada hiyo kwa wanafunzi hao na kwamba benki itaendelea kusaidia huduma za kijamii kila uwezo utakapokuwa ukiruhusu.

 

Akipokea misaada hiyo Mkuu wa mkoa Kigoma,Thobias Andengenye ameishukuru benki ya NMB kwa msaada huo na kuonyesha kuguswa kwake namna benki hiyo inavyojitolea katika kusaidia huduma za kijamii na kuunga mkono serikali katika kusaidia kupeleka huduma kwa jamii.



inakuwa kwa wote lakini pia kuondoa utegemezi kwa watu wenye ulemavu wanapoanza   kujitegemea


wanafunzi wanaosoma na kuishi bweni shule hapo akiwemo  Fatuma Fundikini na Taru Salehe ameshukuru msaada huo wa NMB kwani utasaidia kupunguza changamoto zinazowakabili ingawa wamesema kuwa bado changamoto za mahitaji mbalimbali shuleni hapo ni kubwa.

 

Wametaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na tatizo la ukosefu wa maji safi na salama hivyo kulazimika kutembea kufuata maji mto Bitale jambo ambalo wakati mwingine linaharibu ratiba zao za masomo.

 


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI