NA HAMIDA RAMADHAN DODOMA
SERIKALI imeiwezesha Taasisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali kiasi cha shilingi Bilion 2 kwa ajili ya kununua mitambo na vifaa vya kisasa ili kuboresha uchunguzi wa kisayansi wa kimaabara mwaka wa fedha 2021/2022.
Hayo yalisema jijini hapa na Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt, Fedelice Mafuniko wakati akielezea utekelezaji wa Shughuli na muelekeo wa utekelezaji Kwa mwaka wa fedha 2022/23.
Alisema mitambo ni kwa ajili ya kuimarisha uchunguzi wa kimaabara Kwa lengo la kuendelea kutoa huduma za uchunguzi wa kimaabara Kwa wananchi Kwa haraka na Kwa wakati.
Alieleza katika kipindi cha mwaka wa fedha 2021/2022 serikali kupitia Mamlaka ya maabara imeendelea kiboresha na kuweka Mazingira wezeshi ya biashara ya kemikali nchini.
"Kupitia uingizaji ,usafirishaji na matumizi Serikali imeweza kufanya mapitio ya sheria ya kemikali na kuruhusu biashara kubwa ya kemikali aina Sulphur inayoingizwa nchini Kwa wingi katika mfumo kichele" alisema Mkemia Mkuu Mafuniko.
Aidha Serikali imeboresha na kuweka Mazingira wezeshi ya biashara ya kemikali nchini ambapo idadi ya wadau na shehena za mizigo ya kemikali zinazoingizwa nchini zimeendelea kuongezeka.
" Katika mwaka wa fedha 2021/2022 vibali vya uingizaji wa kemikali viliongezeka na kufikia 63,588 ikilinganishwa na vibali 49234 vilivyotolewa mwaka wa fedha 2020/2022 ikiwa ni ongezeko la vibali 14,354," alisema
Na kuongeza " Mbali na utoaji wa vibali
vya Kemikali mamlaka ya maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali katika kipindi cha mwaka wa fedha 2021/2022 imefanikiwa kusajili wadau wanaojihusisha na Shughuli za kikemikali 1087 ikilinganisha na wadau 1057 waliosajikiwa Kwa mwaka wa fedha ikiwa ni ongezeko la wadau 30," alisema Mkemia Mkuu Dkt Mafuniko
0 Comments